Conclusion yake siyo sahihi kabisa. Kwa vile ulibadilisha spark plugs ndipo transmission yako ikaacha mshituko haina maana kuwa kila mshituka wa transmission unasababishwa na spark plugs tu, ambalo ndilo jibu lako; siyo kweli.
Mshituko wa transmission husababishwa na ama ATF au umeme basi, labda kama meno ya gear mojawapo amevunjika. Kwa vile umeme wa gari unatoka kwenye alternator na kusambaa gari zima, kitu chochote ambacho kinatumia umeme kikila umeme mwingi kuliko mgao wake wa kawaida basi transmission pia itashindwa kufanya kazi vizuri. Hata redio ikiwa na shoti ikawa inakula umeme mwengi sana basi transmission yako nayo itashtuka.
Nadhani wewe ndiye hukunielewa.
Iko hivi, plug moja ilizokuja nazo ilikuwa haichomi, ikawa ina misfire. ODB ikasoma plug ya pili haichomi zikabadilishwa zote.
Siku ya pili ikawa gari kuna muda kama inaslip slip vile. Nikarudi wakachomoa wakaweka nyingien... nayo siku tatu zikaanza kuzingua, nikaenda kwa fundi mwingine.
Akaweka plug nyingine but nimetembea nazo siku hiyo gari ikarudi kuwa kama inaslip tena. Nikaona isiwe tabu ntakaa nazo hivyo hivyo.
Nimekaa nazo miez almost 4, lakini nilienda kwa fundi mwingine akaendesha akasema hii mbona si kama plug hii itakuwa gearbox na hizi cvt ni bora ununue nyingine na hapo nilikuwa nishabadili chase kwenye gearbox kuna sensor ya pressure iliungua nikashauriwa niweke chase nzima badala ya sensor tu.
ODB haikuwa inasoma kuwa transmission ina shida ila ilikuwa inasoma misfire. Ila inavyokuwa inaslip unaweza hisi labda gear haziingii.
Baada ya bwana miraba, kuniwekea plug hizo, misfire ikaondoa, no error code kwenye mashine na gari iko sawa.
So my conclusion, hali niliyokuwa naisikia chanzo ni plug ambazo haziendani na gari.
Sasa kuhusu kuslip kama gear haziingii vile, huenda shida sio transmission na wala haikuwa na shida ila sisi kutokana na tulivyohisi ndivyo tukadhani hivyo.