mashi ga ngoko
Member
- Jul 15, 2018
- 96
- 50
Miezi mitano iliyopita nimenunua gari aina ya Corolla 111 kutoka mikononi kwa mtu,mwezi uliopita ilipata tatizo la kuchemsha na kuchanganya oil na maji baada ya kukikimbia umbali mrefu kutoka Dar - Moro,fundi alitengeneza cylinder head na kuirudishia japokuwa gari likawa halina nguvu.Baada ya hapo wiki mbili zilizopita ilipatwa na tatizo la kunoc engine yaani injini ilikua inagonga,fundi anasema niliendesha bila kuweka oili lakini ukiangalia oil stick inaonyesha oil ipo nyingi tu umeshuka kigogo kwenye FULL lkn fundi anaiambia kuwa haitakiwi kushuka hata kidogo.
Tatizo jingine gari linakunywa maji si mchezo yaani kila niendesha umbali wa KM 40 - 50 ukicheki maji yanakua yamepungua kama kiasi cha nusu lita hivi inanilazimu niongeze wakati wengine nawaona hawaongezi maji mara kwa mara.
Naombeni uzoefu wenu juu ya hili.
Pia naombeni ushuhuda kama kuna mtu alishawahi kupeleka gari lake kwa wachina likiwa na tatizo kama langu naomba msaada wa mawasiliano wanapopatikana na ushuhuda wa kutengenezewa gari lake na kupona,pia gharama nipo tayari kugharamia.