Msaada gari langu linanisumbua

Msaada gari langu linanisumbua

Joined
Jul 15, 2018
Posts
96
Reaction score
50
Miezi mitano iliyopita nimenunua gari aina ya Corolla 111 kutoka mikononi kwa mtu,mwezi uliopita ilipata tatizo la kuchemsha na kuchanganya oil na maji baada ya kukikimbia umbali mrefu kutoka Dar - Moro,fundi alitengeneza cylinder head na kuirudishia japokuwa gari likawa halina nguvu.Baada ya hapo wiki mbili zilizopita ilipatwa na tatizo la kunoc engine yaani injini ilikua inagonga,fundi anasema niliendesha bila kuweka oili lakini ukiangalia oil stick inaonyesha oil ipo nyingi tu umeshuka kigogo kwenye FULL lkn fundi anaiambia kuwa haitakiwi kushuka hata kidogo.
Tatizo jingine gari linakunywa maji si mchezo yaani kila niendesha umbali wa KM 40 - 50 ukicheki maji yanakua yamepungua kama kiasi cha nusu lita hivi inanilazimu niongeze wakati wengine nawaona hawaongezi maji mara kwa mara.

Naombeni uzoefu wenu juu ya hili.
Pia naombeni ushuhuda kama kuna mtu alishawahi kupeleka gari lake kwa wachina likiwa na tatizo kama langu naomba msaada wa mawasiliano wanapopatikana na ushuhuda wa kutengenezewa gari lake na kupona,pia gharama nipo tayari kugharamia.
 
Nachokiona hapo kunanshida katika ipoozaji wabl engine..na kunauwezekano kuna leakage kwenye rejeta au pupes zinazozungusha coolant. Na hyo kuchanganyika maji na oil limenishangaza labda kama ulipita kwenye dimbwi kubwa la maji. Kingine jaribu kununua genuine engine na gear box oil..inaweza kusaidia
 
Kuchanganya ilikuwa ni gasket imetoboka,asante mkuu
 
Mkuu fanya diagnostic test kwakutumia kitu kama computer hivi kujua tatizo lipo wapi, au jaribu ku google ukiweka swali hilo na nina uhakika utapata jibu sahihi na njia muafaka kumaliza tatizo lako na nakushauri usiliendeshe tena ama sivyo utalikaanga tena kwa sababu inaonyesha Oil haipandi na mzunguko wa maji una walakini kwani unaingiliana na Oil kitu ambacho hakitakiwi kabisa
 
Asante mkuu hawa watu wa diagnostic ntawapata wapi?
 
Bila kupoteza muda, kanunue head-gasket mpya uende kwa fundi kuiweka. Imeunguza headgasket na hivyo kuna muingiliano wa maji na engine oil kwenye passage. Ukitaka kuhakikisha kama ni head-gasket, washa gari na ujaze maji hadi juu kisha weka maji nusu kwenye chupa ya maji ya kunywa au hata ya soda ambayo ni transparent na uifunikize hapo kwenye water reservoir tank na ukiona mapovu yanapanda kwenye chupa tatizo ni headgasket imeungua/katika. Ukilazimisha kuendesha uta blow head-cylinder ambayo itakugjarimu zaidi kuliko kubadili hiyo gasket. Kila la heri
 
Asante mkuu.
 
Engine iko vizuri sana kila fundi akiisikiliza anaisifia shida ni matatizo hayo tu mkuu.Huo mswaki ndio kitu gani?

Kuchanganya ilikuwa ni gasket imetoboka,asante mkuu

Nini kinapasua gasket? je C/Head haijapinda? .... tatizo lako la msingi ni oil kuchanganyika na maji na kupelekea gari kutokupoza engine hivyo ukiweka gasket mpya nayo itapasuka? hebu jaribu kukagua seat valves, kagua water pump /timing cover gasket, kagua vizuri hiyo C/Head kama haijapinda, je water pumb ni nzima na haivuji?...kuwa makini na mafundi wetu chini ya mwembe wasikumalizie pesa yako bila sababu ya msingi na jaribu kupata fundi wa kufanya diagnostic test kwanza
 
Miezi mitano iliyopita nimenunua gari aina ya Corolla 111 kutoka mikononi kwa mtu,mwezi uliopita ilipata tatizo la kuchemsha na kuchanganya oil na maji baada ya kukikimbia umbali mrefu kutoka Dar - Moro,fundi alitengeneza cylinder head na kuirudishia japokuwa gari likawa halina nguvu.Baada ya hapo wiki mbili zilizopita ilipatwa na tatizo la kunoc engine yaani injini ilikua inagonga,fundi anasema niliendesha bila kuweka oili lakini ukiangalia oil stick inaonyesha oil ipo nyingi tu umeshuka kigogo kwenye FULL lkn fundi anaiambia kuwa haitakiwi kushuka hata kidogo.
Tatizo jingine gari linakunywa maji si mchezo yaani kila niendesha umbali wa KM 40 - 50 ukicheki maji yanakua yamepungua kama kiasi cha nusu lita hivi inanilazimu niongeze wakati wengine nawaona hawaongezi maji mara kwa mara.

Naombeni uzoefu wenu juu ya hili.
Pia naombeni ushuhuda kama kuna mtu alishawahi kupeleka gari lake kwa wachina likiwa na tatizo kama langu naomba msaada wa mawasiliano wanapopatikana na ushuhuda wa kutengenezewa gari lake na kupona,pia gharama nipo tayari kugharamia.
Peleka "scrap yard" tu.

Hilo gari utakutana lilikuja nyumba. Walio litumia huko wamechoka nalo, aliyekuuzia wewe kalitumia hapa kachoka nalo. Hilo ni "scrap".

Samahani lakini huo ndiyo ukweli.
 
Umemjibu vizuri sana na kwa kutumia fikra zako hizohizo najiuliza sijui na wewe waliokutumia na kukuchoka siku hizi wanakuita scrap?
 
Nini kinapasua gasket? je C/Head haijapinda? .... tatizo lako la msingi ni oil kuchanganyika na maji na kupelekea gari kutokupoza engine hivyo ukiweka gasket mpya nayo itapasuka? hebu jaribu kukagua seat valves, kagua water pump /timing cover gasket, kagua vizuri hiyo C/Head kama haijapinda, je water pumb ni nzima na haivuji?...kuwa makini na mafundi wetu chini ya mwembe wasikumalizie pesa yako bila sababu ya msingi na jaribu kupata fundi wa kufanya diagnostic test kwanza
Ushauri wangu kwa hali ya hiyo engine ajipange kununua engine used Kariakoo,hapo unaweza kuliwa hela za matengenezo na mwisho wa siku tatizo halitakwisha...
 
Umemjibu vizuri sana na kwa kutumia fikra zako hizohizo najiuliza sijui na wewe waliokutumia na kukuchoka siku hizi wanakuita scrap?
Mada hapa ni mimi au gari?

Sikushangai. Ni wengi sana wenye ujinga kama wako JF. Mkiambiwa ukweli na ukiwaingia na kukosa hoja basi mnaanza matusi.

Nimegundua humu JF kuwa wewe ni kati ya wale watoto wa "single mother" ambao kila mwanamme anaeingia ulipolelewa unaambiwa "mwamkie baba'ko".

Punguani wahed.
 
Kwa uzoefu wangu na kukuepushia usumbufu, huyo fundi hajui anachofanya, oil inaweza ikashuka hadi nusu ya dipstick na isilete shida yeyote ile, huyo muongo, kafunga tuppet za cylinder head vibaya (kakosea kipimo cha filler gauge) anasingizia oil. Pili hiyo cylinder head ina compression leakage, again, huyo fundi kaifunga vibaya, ila bottom line, nunua MSWAKI wa engine pale mtaa wa shauri moyo/ Lindi, utaupata hata kwa laki 4 au 5 tu, tafuta fundi mzuri ahamishe vifaa vizima toka kwenye hiyo engine mbovu kwenda kwenye mswaki, vifaa vya kuhamisha ni starter, a/c compressor, water pump, power steering, alternator, throttle bodyn fuel pump nk.
 
Back
Top Bottom