Msaada: Godoro gani zuri?

comfi, tena nchi 8 na 5 by 6. wewe yan full burudani

inavyoonekana mdau wa comfy ni wewe tu. Mpaka na size umeniwekea, kwa kweli umeshine. Sasa Nianze kupambana na bei za suggested godoros. Ila chapa mtu bado sijaielewa.
 
mkuu, bado bachelor.

Kumbe hata kuoa bado !
Wewe godoro si muhimu kiiviiile currently hata ukilalia cushion au kwenye kochi poa tu!
Hiyo pesa ya godoro hamishia kwenye items zingine kama kabati , fridge , capert n.k
 
Magodoro ya Sufu ni poa sana, narudia tena godoro bora ni la SUFU, likichanika unashona, unaweza kushonea ka kitambaa kadogo likawa kama kibubu cha kuhifadhia shekeli, ukiwa na sufu huna hofu ya kuvamiwa na vibaka kwa kua watakuona mlalahoi kumbe umenyesha balaa. Na hapo utafanikiwa kupata usingizi mnono utakaokufanya uote.
Ahsante.
 
Duh! JF kiboko! Afu yanauzwa msamvu karibu na round about eeh? Ngoja na mie nitawekeza
 
Tanfoam ni mwisho wa kila kitu.
yaani nlikuwa naskilizia kama Tanfoam itatajwa, hatimae umetokea. Bila kujali uzito wako, umelitumia kwa muda gani, na matokeo yake yakoje?
 
yaani nlikuwa naskilizia kama Tanfoam itatajwa, hatimae umetokea. Bila kujali uzito wako, umelitumia kwa muda gani, na matokeo yake yakoje?

Wala sikifichi kama unania ya kununua godoro katafute Tanfoam. Uwe makini sana wanachakachua haya magodoro. Tanfoam huwa hawachanganyi magodoro yao na mengine, hapa na maanisha " only Tanfoam" wanakuwa na aithorized dealer wao tuu kwa magodoro ya Tanfoam tuu...

Kwa upande wa muda niliolitumia hata sijui ni miaka mingapi...ila inaweza fika kama 12 hivi halafu kitu bado kipo imara...
 
12, aisee hilo ni noma. Hv hilo ndo la babu mpaka mjukuu ama?
 
Kama upo Dar nenda HSC kule Ben Mkapa k'koo, jamaa wana magodoro poa sana...unajua kuwa ukikosea kununua godoro unahatarisha afya yako pia?
 
Hivi unataka godoro godoro au godoro chapa mtu?

Sasa hapo mkuu ndo umefanikiwa kunichanganya kabisa.
Hebu fafanua kidogo kuhusu hilo la ili, maana godoro godoro nalifahamu, sasa hilo chapa mtu badi niko kwenye mataa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…