Ni miongoni mwa shule nzuri sana kwa hiyo comb kwa hapa Bongo,akifika mizani ya Tanga aombe ashushwe kituo kiitwacho Majani mapana,akishuka hapo kama hana mizigo mingi anaweza kutembea kwa miguu au bodaboda ni 1000/= tu, kwa mantiki hiyo shule ipo mjini,nakumbuka enzi hizo tukiita Galax tulikuwa tukitembea kutoka shuleni hapo hadi Usagara sekondari(hosteli zao) kubadilishana hili na lile na ndugu zetu wa pale.ambapo usagara hosteli ni kama mita 160 toka stendi kuu ya TANGA JIJI.HIVYO NI rahisi kukutana na wanafunzi wa USAGARA,TANGA TECH(Shule kongwe YA SERIKALI kuliko zote TANGANYIKA) hvyo kama atatumia fursa nzuri na konection na hzo shule kufaulu BAM nadhani itakuwa rahisi sana kwake shule hizo ni PCM zaidi.Walimu wengi pale ni wazuri sana coz mazingira ya kazi ni pendwa sana.Wakuu naomba msaada wenu. Mdogo wangu kachaguliwa kwenda Form V (HGE) huko Galanos high school, Tanga.
Kuna yeyote anayejua kama shule hii ina mazingira mazuri ya kusoma hiyo combination ya HGE? Namaanisha kama kuna walimu wazuri na mazingira mengine ya kielimu yanayoweza kumfanya mwanafunzi afanye vizuri kimasomo.
Pia naomba kujua shule hii iko maeneo gani, ni hapo Tanga mjini au wilayani? Naomba msaada wenu.