Msaada hii movie ya Suniel Shetty inaitwaje?

Ruyama

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2019
Posts
367
Reaction score
563
Movie inaanza Sunil Shet anaishi na mama yake hawana pesa ikabidi Sunil Shet amuage mama yake, kisha akaenda kumuaga girlfriend wake ambaye kwao ni matajiri.

Baada ya miaka kadhaa wazazi wa demu wa Sunil Shet waka mpa binti yao Akshay Kumar amuoe binti alikuwa hana sauti juu ya wazazi wake.

Mzee mzima Sunil Shet akawa amesharudi kuhaso akafanikiwa kupata pesa nyingi akawa Don kwa bahati mbaya mama yake akafariki akachomwa moto.

Basi Sunil Shet (Devi jina alilotumia) akaenda kwao na demu wake akaambiwa ameshaolewa na kijana mfanya biashara Sunil Shet akachanganyikiwa akamfatilia hadi Delhi.

Akafanikiwa kukutana na demu wake hakuamini kumuona msela aliyeachana nae na kwenda kutafuta maisha
 
Hiyo movie inaitwa dhadkan noma sana,,
Hao jamaa joint zao znakuaga sio poa..
Bonge moja la movie yani..
 
Yea hii muvi kazi. Kinachoniuma ni muvi ambayo niliiangalia enzi za Lufufu kibandani Big M na sijawahi itafuta sasa hivi ili niielewe.

Disco Dancer nilishindwa vumilia nikaitafuta. Vishwatma haipo online, Sholar aur shabnam haipo online pia ila ilitakiwa nizipige review
 
Hii movie LUFUFU hakuwahi kuitafsri
Hii MOVIE kipindi inatoka LUFUFU miaka ya elf 2000 mwanzoni LIFUFU alikuwa ndio anaacha kutafsiri MOVIE so hii movie hakuwahi kudeal nayo
 
Kwahiyo unanipinga?

Muvi za miaka ya 2000 ni hizo Jaan Dushman. Hii ni ya kitambo.
JAAN DA DUSH MAN imetoka 2002
Hii imetoka 2000
Na song kali katika hii MOVIE lenye huzuni mno kukalibia mpk kutoa machozi
Linaitwa DIL NE YE KAHA HAI DIL SE
mtoto anamlila MTAMBO wa KULEKEBISHA tabia(suni shetty)
Lkn baadaye anakumbuka aneshaolewa haiwezekani tena na Wahindu ukishaolewa ni km ndoa ya KIKATORIC ndio wako milele
Hapo songi linapokolea Sunil shetty kalalamika sana tena sana WAHINDI noma sana

 
Ilo songi limepigwa kama dakka 10 yani af linavyoendelea unakuta linakuchkua linakupeleka mbali sana,
Hii movie ina mixed filling sana unajkuta inakuchkua t bila kupenda,
 
Rufufu mungu anamuona aisee.. Sunil Shet yeye alikua anamuita Shurusheti.

Kuna muvi inaitwa Tere naam ya Akshay bonge moja la muvi. Napenda sana Bollywood movies sema sina pa kuzipata mpaka nikiwa na muda niangalie B4U movies. Nina nyimbo za kihindi 500 zote video usiku napenda kulala nazisikiliza
 
Juma Khan acha miyeyusho.

Mimi nimeangalia hii muvi kwenye banda la video. Big M Mwananyamala kwa Kopa. Ikiwa imetafsiriwa.
 
TErE Naam - Salman Khan
 
Ha pole mkuu mkuu ungekuwa DAR ungekuja nikakupa tu nina kama zote kunzia miaka ya 2010 kushuka chini hasa 90s na 80s ila ninazo mpk za miaka 60 baadhi

 
TErE Naam - Salman Khan
Yeah
tere naam ya SALMAN KHAN mpk anakuwa chizi 7bu ya demu

AKSHAY KUMAR na RAVEENA TANDON
hawa ndo walonifanya niwe mpenzi wa MOVIE za KIHINDI tangu miaka ya 94 95 hivi TV zilipoanza kuwa nyingi BONGO

katika MOVIE za miaka ya 2000 ninayokubari ya AKSHAY kuna KHAKEE humo kaupiga mwingi na AMITABH BATCHAN pamoja na AJAY DEVGAN kama kawaida Kupenda MADEM ndiko kulimponza katika MOVIEE hii
bila kusahau AJNABEE humo anacheza na BOB DEO ni baadhi ya MOVIE chache za miaka ya 2000 ambazo ndio walikuwa wanamaliziamalizia ule ubora wao
Enzi hizo

Now demu hazeeki aisee
 

Attachments

  • Screenshot_20210702-225758_Facebook.jpg
    31.3 KB · Views: 10
Kakhe si ndio walikua wanampeleka mtuhumiwa somewhere aksha akanaswa na honeypot ya mdada aliyejifanya anamatatizo adui ni ajay mwenyewe.
Au nimechanganya na Mr indian ya Suny deol..
Niliiona kwenye ST bollywood swahili
 
Kakhe si ndio walikua wanampeleka mtuhumiwa somewhere aksha akanaswa na honeypot ya mdada aliyejifanya anamatatizo adui ni ajay mwenyewe.
Au nimechanganya na Mr indian ya Suny deol..
Niliiona kwenye ST bollywood swahili
Ndio hiyo mzee mwenzangu AKSHAY anakufa katika uwanja wa mpira
Naikubari sana ile MOVIE
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…