Msaada hii movie ya Suniel Shetty inaitwaje?

Bonge moja la story, songi lake ni la [emoji91]

Kuna baadhi ya movie wahindi wametuliza kichwa, shida huwa ni kwenye action tu [emoji23][emoji1787]

Nimecheki movie nyingi za kihindi uchawi majina siyajui.
 
DARR,
hii muvi amecheza sharukhan na sunny deol..
katika muvi zenye songs kali basi darr haitakosekana..

storyline..
sharukhan alikuwa anampenda mwanamke(juhi chwala)ile kufa.
hadi ikampelekea tatizo akawa(socialpath au chizi mapenzi)ajabu toka chuoni wakisoma jamaa alikuwa domo zege kumtokea demu na kumwambia anampenda.

maisha yakaenda jamaa akizidi kuteseka huku yule demu alikuwa tayari na mchumba(sunny deol)ambae alikuwa mwanajeshi wa majini.baada ya kuwa mwanamke kamaliza chuo mikakati ya uchumba na kufunga ndoa ikawa imeshika kasi.

huku sharukhan akiteseka na kuwafanyia vituko ambavyo sio vya binadam mwenye akili timamu..
alidhamiria kuua mtu yoyote atakaemsogelea yule manzi.
hapo akakutana na mbabe sunny deol.
ingawa aliteswa sana lakini mwishoni aliweza kumuua sharukhan.

ni muvi tamu sana.ingine KOYLA.
muvi za zamani zilikuwa na stori nzuri sana halafu zinaeleweka hata km hujui kigabachori
 
ROWDY RATHORE..
akshay kumar akiwa ni askari jasiri na shupavu aliweza kumaliza tatizo la ujambazi katika eneo alilopewa majukumu...
sifa zake zilitamalaki katika ngazi zote za jeshi.
hii ilipelekea ahamishwe sehemu nyingine ambapo alienda kukutana na mambo hakuyategemea!
siku amefika katika kituo cha kazi akiwa na mwanae wa kike aliposhuka kwenye tren tuu wakora wakamfata wakitaka pesa bila kujua ni mtu gani.
aliwatandika na miwa hadi wakajinyea kisha akachukua pesa zao na kuwarudishia raia walioporwa!!
akiwa amepokelewa na askari walio chini walitambua kwamba akshay alikuwa amefiwa na mke wake...

katika wale askari wake mmoja aliulizwa na akshay wee mkeo yuko wapi naona unaishi tuu na watoto..!
akaogopa kusema hadi watoto wakasema kwamba mama ametekwa!

yule askari akamwelezea kwamba kuna DON hapo kijijini amemteka mke wake na kila akienda kumdai anaambiwa arudi baada ya siku 3...yaani kibabe unamuona mke wako analiwa halafu unaambiwa njoo baada ya mda umchukue..jamaa kinyonge anaondoka..

hapo ndio visa na mikasa inaanza!
ni muvi nzuri sana.
 
usipomtaja amrish puri utakuwa hujaitendea tasnia haki kabisa...
zamani wadogo ukikataa kula tuu unaambiwa amrish puri anakuja mbona msosi utaisha huo..hahahah
Koyla. Makaa ya motoooooo.
 
Kuna muv moja inaitwa QAYAMAT umo ndan kacheza AJAY DEVGAN na SUNIL SHETTY muv balaaa sana hii Ajay alifungwa gereza ambalo miaka 1000 hajawah kiumbe yyt kutoroka kaenda yy kakaa miez3 katoroka akawafata walomsababishia kesi akawaua then akapelekwa tena jela baadae Sunil atahitaj msaada wake kuna manyamela wanasuka mipango ya kurusha nuclear kutoka katika hilo gereza asee mziki wake co wa kitoto kuna song moja Matata sana Ajay anakumbuka wakat anapelekwa uko kuwasaidia polis linaitwa Diljual Lia(sina hakika kama ni sahih)
 
usipomtaja amrish puri utakuwa hujaitendea tasnia haki kabisa...
zamani wadogo ukikataa kula tuu unaambiwa amrish puri anakuja mbona msosi utaisha huo..hahaha
Koyla. Makaa ya motoooooo.
hii dada alitupwa kwenye mto wa mamba anaitwa REKHA na muvi inaitwa KHOON BARI MAANG..
jamaa aliamua kumuua mke ili ale bata vizuri na mchepuko.huku akitumia mali na ukwasi wa mke wake.
 
Shahrukh hiiii mkuu. Shahrukh alilishwa makaa ya mawe ili asiseme mauaji ya wazazi wake maana aliona wakiwa wanauliwa
 
Shahrukh hiiii mkuu. Shahrukh alilishwa makaa ya mawe ili asiseme mauaji ya wazazi wake maana aliona wakiwa wanauliwa
aliemlisha hayo makaa ndio amrish puri..
baba ake na sharukhan alipata madini ya thamani akamuonesha ndugu yake ambae ni amrish.kwa tamaa amrish ndio akamuua kisha kumlisha makaa ya mawe mtoto wa kakaake ambae ndio sharukhan!
kisha akawa anamtumikisha km mbwa wake!
amrish akiwa hapati msisimko kwa mke wake hivyo mganga wake wa mitishamba akamshauri atafute binti mwingine mdogo mbichi amuoe ndio hamu yake itarudi.
katika pitapita zake ndio akamuona yule binti maskini(madhuri).akatumia ushawishi wake wa pesa kisha akamuoa kwa nguvu!!
baada ya sharukhan kugundua jinsi yule binti anapitia mateso ndio akaamua kutoroka nae!kumbuka binti wakati anachumbiwa alionyeshwa picha ya sharukhan sio amrish hivyo akakubali!!

hapo ndipo shughuli pevu ikaanza hadi kufikia bubu kuongea...
 
Dhadkan Sunil,Akshay na Shilpa Shetty nawaelewa Sana hawa watu
 
Hizo movie Star Gold hua wanaonesha sanaaa!Haswaa Sholay!naielewa sana hii movie
 
Teree naam ya Salmaan Khan Bwana!Bhaijaan anakuwa chizi
 
Khakee first time nilivoiangalia nililia aseehh!!!Mimi bwana kwa wahindi nalia kama mtoto Niko too emotional!!! Halafu nampenda Devgan ndo kawa adui daahh!Aishwarya Rai mule ameact vzr sana
 
Ndio hiyo mzee mwenzangu AKSHAY anakufa katika uwanja wa mpira
Naikubari sana ile MOVIE
Aishwarya anampiga risasi Akshay bila huruma aseehh!!!Mchizi anamuambia Demu amuue si anaumuua kweli!!Dada gaidi then bwana ake Ajay Devgan
 
usipomtaja amrish puri utakuwa hujaitendea tasnia haki kabisa...
zamani wadogo ukikataa kula tuu unaambiwa amrish puri anakuja mbona msosi utaisha huo..hahahah
Sisi Daslama tulikua tunamuita mzee Ashanti daah huyu baba acha kabisaa
 
Kuna movie ya Hollywood nafkiri walichkua hio story.

Zamani movie nyingi za kihindi walikuwa wanachkua story za kizungu. Sema wao huongeza na manjonjo na nyimbo zao zile basi story huzidi kuwa tamu
 
Mie nikiangalia movies za wahindi huwa nalia tu.

Huo disco dancer niliangalia mara nyingi lkn kila nikiangalia nilikuwa nalia [emoji23]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…