Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Nime-attach picha,ni hali ambayo siilewi ..yani tikiti inakuwa kama inakauka sijui inakuwaje..hiyo ni nini jamani na naidhibiti vipi?????
KIONGOZI POLE KWA HIZO CHANGAMOTO,
NAOMBA NIFAHAMU YAFUATAYO ILI NIWEZE KUJUA CHANZO CHA HILO TATIZO NI NINI
1. HALI YA HEWA YA HILO SHAMBA MCHANA INAKUWAJE NI JOTO SANA (JUA KALI SANA??) NA USIKU KUNA KUWAJE????
2. UDONGO WAKO NI WA AINA GANI (KICHANGA) KAMA MCHANGA WA KUJENGEA?? AU NI ULE MWEKUNDU, AU NI ULE MWEUSI (MFINYANZI??)
3.UMEWEKA MBOLEA ZIPI NA ZIPI MPAKA SASA, YAANI TANGU ULIPOPANDA MPAKA SASA??
4. UNAMWAGILIA MARA NGAPI KWA WIKI??
5. KUNA DAWA ZIPI ZA UKUNGU/WADUDU UMESHAPIGA MPAKA SASA??
6. NAOMBA KUJUA MAJANI YA MMEA YAMEATHIRIKA PIA (ie kujikunja/au unjano au madoa doa??)
ASANTE, TUKIFAHAMU HAYO TUNAWEZA KUFIKA KATIKA HITIMISHO SAHIHI
POLE
1.Hali ya hewa wakati wa mchana huwa ni jua na usiku huwa na baridi fulani hivi ambapo wakati mwingine asubuhi huwa na umande..
2. Udongo ni mweusi lakini si mfinyanzi..ni tifutifu mchanganyiko na mchanga.
3. Mbolea: Nimepanda na DAP ,nimekuzia na Yara Winner, na badae nikaweka Nitrabor(as CAN).
4. Namwagilia kila baada ya siku 4.
5.Dawa ni nyingi nilizotumia..ila kwa ufupi;kwa ajili ya ukungu ninetumia Ridomil,Bluecopper na Mupavil.. kwa ajili ya wadudu nimetumia KARATE,ATTACKAN,na SPIDEX.
6.Kuhusu majani yako vizuri..isipokuwa huwa kuna moja moja naona kuwa ya njano na machache yamejikunja.
HABARI, HII HUDUMA YA USHAURI UNAUTOA KWA GHARAMA? KAMA NDIO NI KIASI GANI? NINGEPENDA KUKUULIZA KUPITIA EMAIL YAKO VITU VIWILI VITATU KUHUSIANA NA KILIMOSAWA MKUU NIMEKUPATA
MARA NYINGI SHIDA KAMA HIYO HUSABABISHWA NA MAMBO MAKUU MATATU
1. WATER STRESS/SUN BURN=KAMA JUA NI KALI SANA NA MMEA UKO NA MATUNDA, NA MAJI NI KIDOGO NA JOTO NI KALI SANA, KWANZA UTAONA MMEA UNAPUKUTISHA SANA MAUA, PAMOJA NA MATUNDA KUUNGUA KWA KUPIGWA NA JUA/KUCHOMWA NA JOTO TOKA KATIKA ARDHI. INASHAURIWA TIKITI ZIKISHA FIKA SAZI KAMA HIYO YAKO BASI CHINI UWEKE MATANDAZWA MENGI ILI KUABSORB LILE JOTO LAKINI PIA MAJI YASIKOSEKANA WALAU MARA 1 KILA BAADA YA SIKU 1.
2. SABABU YA PILI AMBAYO HWEZA KUSABABISHA TUNDA KUOZA/KUBABUKA NGOZI NI UPUNGUFU WA MADINI YA Calcium (Ca), ambapo husababisha ganda la tunda kuwa dhaifu, ndio maana hata kuku hupewa madini ya chuma/vyakula vya chumvi chumvi na michicha ili kuimarisha mayai (lile ganda la yai ni Calcium), Calcium ikikosekana hata katika matunda, ganda la tunda huwa dhaifu sana. Calcium na maji vikikosekana tunda huoza chini ya kitako (Tatizo huitwa Blosom end rot)
View attachment 389661
3. SABABU YA TATU inayoweza kusababisha tunda kuwa hivyo ni madhara ya wadudu, hasa Fruit borer/Fruit flies, hutoboa tunda kwa juu au chini, na kisha ile sehemu huoza, na ikishaoza inakuwa madharia ya bakteria na fungus huingia hapo na tunda lote huoza
View attachment 389665
SULUHISHO
=Weka maji angalau mara 1 kila baada ya siku 1
=tumia dawa kama vile buffalo au Match au Nimbecidine dhidi ya wadudu watoboa matunda
=Weka matandazwa chini ya matunda, kuzuia yasichomwe na fukuto la joto toka katika ardhi/udongo
==================
HABARI, HII HUDUMA YA USHAURI UNAUTOA KWA GHARAMA? KAMA NDIO NI KIASI GANI? NINGEPENDA KUKUULIZA KUPITIA EMAIL YAKO VITU VIWILI VITATU KUHUSIANA NA KILIMO
Sawa asante..karibu
tuna uzi wetu ambao uko sticky katika hili jukwaa unaweza kuufuatilia kutokea hapa chini
Je, unataka kulima mazao ya mbogamboga na matunda lakini unakosa maarifa sahihi?? Karibu tushauriane
KAMA UNAMASWALI UNAWEZA KUULIZA TU HATA HAPA OPEN AU KWA E-MAIL SAWA, KAMA UTATAKA UWE NA SISI KIKAZI, PITIA HIYO LINK HAPO JUU
Vipi mkuu ulifanikiwa baada ya kutumia hizo dawa ama tatizo liliendelea. Matikiti yangu yamekumbwa na hali hiyo pia.Nashukuru Bwana Kilimo Maarifa...kwa namna moja au nyingine umenipa suluhu ya hilo tatizo..