Msaada: Hivi JamiiForums ni Corporate entity?

Msaada: Hivi JamiiForums ni Corporate entity?

bnhai

JF-Expert Member
Joined
Jul 12, 2009
Posts
2,832
Reaction score
2,390
Ninauliza kufuatia tukio la Bw. Max huku nikilinganisha na lile lilitokea la Apple kule Marekani.
Kama JF ingekuwa kampuni with limited liability, Max angekamatwa au kampuni ndio ingeshtakiwa?
Kule Marekani baada ya FBI kutaka kuchunguza simu za watu waliohusika na ugaidi, Apple walikataa kuwaelekeza namna ya kuhaki simu zile. FBI wakaanza taratibu za kupeleka shauri lile mahakamani mpaka ilipojitokeza kampuni yenye uwezo wa kuhaki. FBI walikuwa wanataka kibali na kwa kuwa ni kampuni hakuna ambaye angeguswa. Sina hakika kwa sheria zetu, njia hii inaweza kutumika?
 
Mahakama ndio itatafsiri sheria na ndio kazi yake.
 
Sawa , lakini kuna wabobevu sheria humo Jf hebu tafadhali mtujuze juu ya hili.
 
Kama malawyer wa max wapo vizuri
Max hakawii kutoka jela akiwa bilionea aiseee
Our Police has to learn to respect laws
 
Maswala ya limited liability, sole proprietorship kwa polisi ni misamiati migumu na wala hawajui sheria zake
Whether JF ni corporate entity au la, kumbuka tu ile VEIL DOCTRINE, au mwavuli unaomkinga mtu against mashtaka huweza kuondolewa na akashtakiwa kwa manufaa ya UMA. ref case ya NURDIN AKASHA.
 
Hii ishu naweza toa maelezo lakn daa ebu tuliache kama lilivyoo,,
 
Back
Top Bottom