Kuna dada yangu ameathirika, ametumia ARV toka 2007 na anafuata masharti vizuri sana. Mumewe alifariki yeye alishindwa kukubaliana na matokeo, hajaolewa hadi sasa ila mpenzi anae lkn ye condom anaziombaga hospital wanampaga box zima. Na akitoka na mpnz wake anabeba kwenye pochi condom zake. Kwa kweli anajijali sana, hata hosp huwa wanamtumia km role model kwa wagonjwa ambao wanatumia ARV lkn afya zao bado hazijaimarika.
Toka mwaka juzi mwanzoni, CD4 zake zilikuwa juu sana, wakamwachishia ARV lkn clinic km kawaida, baadae wakamwambia aende kila baada ya miezi 2 clinic akawa anafanya hivyo, baadae wakachukulia damu na wenzie wengine walioteuliwa ikapelekwa muhimbili kwa vipimo. Majibu yakaonesha kwenye mzunguko wa damu hamna virus, wameambiwa watapimwa tena baada ya miezi sita. Lkn hadi sasa hanywi dawa lkn clinic anahudhuria na ameambiwa akihisi kuumwa chochote awahi haraka hospital. Kwa hiyo ye hata akiumwa mafua anakwenda CTC. Hivi baadae haiwezi kumletea shida hivyo anavyokaa muda bila kunywa dawa, ingawa ni kwa maelekezo ya madaktari na CD4 zake hadi leo ziko juu sana