Msaada: Huu ni ugonjwa gani?

Msaada: Huu ni ugonjwa gani?

Hakuna anayejali

JF-Expert Member
Joined
Jun 3, 2023
Posts
418
Reaction score
526
Msaada tafadhali hii ni homa gani na dawa yake nini?

IMG_20230727_115248.jpg
 
Msaada tafadhali hii ni homa gani na dawa yake nini?
Wewe kuna sabuni au vipodozi umetumia vimekudhuru tafuta Daktari wa magonjwa ya ngozi akusaidie ubaya hio ipo ndani ya ngozi na ishafika kwenye mzunguko wa damu yaani hapo unaenda kupatiwa dawa ya kupaka na kumeza ili kuuondoa huo ugonjwa wako, angalieni na vipodozi mnavyopaka wakati mwingine sio kila sabuni ni rafiki kwa ngozi yako
 
Usitumie kemikali kwenye mwili wako bila kuzijua vizuri. Kabla ya kuingiza kitu chochote kipya kwenye mwili wako, hata kama ni chakula au kinywaji, jaribu kufanya utafiti uone ni nini kinaweza kukupata pamoja na kufuata ushauri wa wataalamu wa kitu husika.

Ungeeleza historia na ni nini unachodhani kuwa chanzo cha ugonjwa huo, ungepata msaada zaidi.

Lakini usije kamwe ukatumia jukwaa hili kuuliza na kufuata ushauri wowote kama njia sahihi ya kujipatia matibabu. Utakufa kabla ya wakati wako.

Mwisho nishauri uzi huu ufutwe. Nionacho ni kuwa muuliza swali siyo mwenye tatizo. Itakuwa kachukua picha ya mwenye ugunjwa bila ridhaa yake na kinyume na maadili ili kujipatia habari na umbea kwa maslahi yake binafsi anayoyajua.
 
Back
Top Bottom