Kwa kweli nadhani huyu dada atakua ana tatizo kisaikolojia na inawezekana limeanzia kwenye hiyo familia yao! Atafutiwe mwana saikolojia ili aweze kumpa msaaada, maana katika hali ya kawaida mtu mwenye akili timamuhuwezi kufanya hivyo.
Asiitoe hiyo mimba maana itazidi kumpa wakati mgumu! Pia, kama wadu walivyo comment, inaelekea jamaa hamjali na ndio maana anamuambia atoe mimba hovyo hovyo! Maana mi naamini huyo mwanaume angekua anajali basi angelazimisha kutumia kinga ili asimtundike mimba nyingine. Kwa vile ameona binti ni mdhaifu anatumia huo mwanya kumkandamiza.
Pia binti asilazimishe penzi, mtu mwenye nia na wewe hatasubiri kulazimishwa akajitambulishe, atafanya hivyo bila kushinikizwa hapo hamna mapenzi kabisa!