Msaada: Huyu ni nyoka wa aina gani?

Msaada: Huyu ni nyoka wa aina gani?

The unpaid Seller

JF-Expert Member
Joined
Oct 27, 2019
Posts
2,113
Reaction score
6,251
Peace,

Wakuu jirani yangu amekua ananiambia hua anamwoma nyoka mkubwa nyakati za jioni akikatiza katika uzio wake. (Uzio unaotutenganisha) awali nilidhani ananitania maana manawake huwa waoga waoga tu akiona kijiti anaweza kusema nyoka au pia utani na masikhara

Lakini kwa umri wake sio mtu wa utani (mama mtu mzima) aliponiambia mara ya pili na ya tatu nikaanza kua makini. Sasa leo jioni hii upande wa pili na kule anakoniambia nimekutana na huyu nyoka nikamuua.

Nilipomuita aje kumtazama akasema nyoka anayemuonaga ni kama huyu kwa muonekano ila mkubwa zaidi, akasema ni kama mara 3 kwa unene na urefu hana uhakika maana hua hamuoni mwanzo mpaka mwisho wake.

Wakuu hapa naona sasa nahitaji kukaa mguu sawa maana ni kama kuna kambi ya hawa viumbe maeneo haya tuna share oxygen pamoja. Huyu niliyemuua anaweza kuwa mtoto wa huyo anaeonekana. Hapa kutakua na kiota.

Wakati najipanga kuwakabili hawa wajomba naomba aliye na ufahamu wa aina za nyoka anifahamishe huyu ni aina gani ya nyoka na tabia zake na je natakiwa kukabiliana nao katika mtindo upi.

(Najua utaratibu wa kuwataarifu mamlaka ya maliasiri lakini wote tunaifahamu nchi yetu kama ghorofa la Kishimba lilipoungua wakataarifiwa jeshi la zima moto sio tu walikuja siku iliyofuata yani walifika baada ya masaa 32 ila pia walikuja na gari halina maji, unaweza ukapata picha kuwategemea mamlaka za serikali ilivyo risk
20240403_203608.jpg


Update: Nimelazimika kuihamisha familia (mke, watowo watatu na dada wa kazi) hapa nitabaki mwenyewe mpaka vita na hawa viumbe itakapofika tamati, maana kuna kila dalili huu mziki utakua bab kubwa. Hapa kutakua na kiota
 
Nyoka hana shida kama hujamchokoza
 
Ingekuwa vizuri kama ungepiga picha kwa utulivu kichwa chake kikiwa kinaonekanavizuri. Hapo ni ngumu kumtambua kwa rangi maana wengi wanafanana kutokana na mazingira wanaoishi.

Pia ungesema makazi yako yako wapi ili tujue tabia nchi ya eneo na aina ya nyoka wanaopatika na katika mazingira hayo
 
Asante mkuu, kwa bahati mbaya kichwa chake nilikiponda kabisa wakati nakabiliana nae. Ila hapa ni Morogoro
Ingekuwa vizuri kama ungepiga picha kwa utulivu kichwa chake kikiwa kinaonekanavizuri. Hapo ni ngumu kumtambua kwa rangi maana wengi wanafanana kutokana na mazingira wanaoishi. Pia ungesema makazi yako yako wapi ili tujue tabia nchi ya eneo na aina ya nyoka wanaopatika na katika mazingira hayo
 
Back
Top Bottom