Msaada: Huyu ni nyoka wa aina gani?

Msaada: Huyu ni nyoka wa aina gani?

Anakula sana panya na mijusi, wengi husema kuwa hana madhara... Lakini usiamini katika hilo linapokuja suala la hawa wadudu
Suala la NYoka linategemeana pia na mazingira mfano green water snake wanauwawa sana kufananishwa na green mamba au boomslangs madume ila kiufupi NYoka hawana shida ukifata mambo zako

Ile mambo ya vitabu vya dini kusema NYoka ni shetani imetumaliza watu weusi
 
Pole na hongera kwa kufanikiwa kumdhibiti. Nadhani anaweza akawa black mamba/koboko.

Njia ambayo nimewahi kuitumia kudhibiti nyoka ni kumwaga mafuta machafu kuzunguka nyumba yote na baadhi ya maeneo ambayo unahisi wanaweza kuwepo.
nashukuru kwa ushauri mkuu, lakini kuna mvua sana nyakati hizi hata hapa mda huu kuna kama manyunyu, je kunaga mafuta itakua mbinu yenye matokeo ya kudumu ?
 
Wakati najipanga kuwakabili hawa wajomba naomba aliye na ufahamu wa aina za nyoka anifahamishe huyu ni aina gani ya nyoka na tabia zake na je natakiwa kukabiliana nao katika mtindo upi.
Mboni umempigapiga sana hivyo huo ni unyanyasaji wa haki wanyama ni Sawa ukamkuta Mbwa mkali anakatiza barabarani ukaamua kumgonga ili umvunjevunje Miguu wakati hajakufanya chochote, ngoja kwanza niwashe Skanka nakurudia

Huyo nyoka umemuua Ila hajawahi kukufanya chochote uenda ndio ulinzi wako wewe unaamua kuua wakati wanakulinda, tangu uambiwe hawajawahi kukufanya chochote inamaana hawapo kwa ajili ya kukudhuru Ila wewe unajishtukia tu mkuu, usiue viumbe hivyo navyo vinahitaji kuishi tafuta watu wa maliasili waje kuwaondoa Ila kuwaua Si Jambo jema Mimi sijafurahia in short imeniuma sana kuona ulivyomuua huyo nyoka yaan hapa naandika machozi yananilenga najipoza na Skanka kukazia machungu uliyomfanyia huyo nyoka just imagine ungekua wewe ndio umepondwapondwa hivyo ungefurahia?
 
Suala la NYoka linategemeana pia na mazingira mfano green water snake wanauwawa sana kufananishwa na green mamba au boomslangs madume ila kiufupi NYoka hawana shida ukifata mambo zako

Ile mambo ya vitabu vya dini kusema NYoka ni shetani imetumaliza watu weusi
Ni kweli lakini kuna huyu uliyemtaja green water snake na boomslangs kiasi fulani wanafanana... Sasa ukikutana nae mara ya kwanza unaweza ukajichanganya... Na kujichanganya kwa boomslangs ni mwanzo wa kuandaa matanga... sababu Hakuna dawa ya kuondoa sumu ya boomslangs
 
nashukuru kwa ushauri mkuu, lakini kuna mvua sana nyakati hizi hata hapa mda huu kuna kama manyunyu, je kunaga mafuta itakua mbinu yenye matokeo ya kudumu ?
Wala hamna shida, mafuta machafu yatafukuza nyoka wote hata kwa harufu tu. Nyoka na mafuta hawapatani na pia mafuta ni njia nzuri ya kudumu.
 
Haonekani vizuri japo rangi yake ni kama black mamba
 
Amekaa kama koboko (black mamba)
 
Peace,

Wakuu jirani yangu amekua ananiambia hua anamwoma nyoka mkubwa nyakati za jioni akikatiza katika uzio wake. (Uzio unaotutenganisha) awali nilidhani ananitania maana manawake huwa waoga waoga tu akiona kijiti anaweza kusema nyoka au pia utani na masikhara

Lakini kwa umri wake sio mtu wa utani (mama mtu mzima) aliponiambia mara ya pili na ya tatu nikaanza kua makini. Sasa leo jioni hii upande wa pili na kule anakoniambia nimekutana na huyu nyoka nikamuua.

Nilipomuita aje kumtazama akasema nyoka anayemuonaga ni kama huyu kwa muonekano ila mkubwa zaidi, akasema ni kama mara 3 kwa unene na urefu hana uhakika maana hua hamuoni mwanzo mpaka mwisho wake.

Wakuu hapa naona sasa nahitaji kukaa mguu sawa maana ni kama kuna kambi ya hawa viumbe maeneo haya tuna share oxygen pamoja. Huyu niliyemuua anaweza kuwa mtoto wa huyo anaeonekana. Hapa kutakua na kiota.

Wakati najipanga kuwakabili hawa wajomba naomba aliye na ufahamu wa aina za nyoka anifahamishe huyu ni aina gani ya nyoka na tabia zake na je natakiwa kukabiliana nao katika mtindo upi.

(Najua utaratibu wa kuwataarifu mamlaka ya maliasiri lakini wote tunaifahamu nchi yetu kama ghorofa la Kishimba lilipoungua wakataarifiwa jeshi la zima moto sio tu walikuja siku iliyofuata yani walifika baada ya masaa 32 ila pia walikuja na gari halina maji, unaweza ukapata picha kuwategemea mamlaka za serikali ilivyo riskView attachment 2953224

Update: Nimelazimika kuihamisha familia (mke, watowo watatu na dada wa kazi) hapa nitabaki mwenyewe mpaka vita na hawa viumbe itakapofika tamati, maana kuna kila dalili huu mziki utakua bab kubwa. Hapa kutakua na kiota
Huyo ni kitukuu Cha anaconda msubiri anaconda mwenyewe
 
Sasa boomslang ni hatari maana Hana ant venom na pia sio rahisi kukudhuru manake ni back fanged yaani Ili a inject sumu yake lazima akuume na meno ya nyuma
Kitu ambacho ni kigumu sana labda wakati anawinda vinyonga na ndege

Maana yeye ni mpanda miti,Hawa nimeshiba sana wakati navuna kahawa Moshi huko!
Ila hakuna NYoka asiyeng'ata ila asilimia 35 ndio Wana sumu na hao ni vigumu mno kuuma mtu

Ni kweli lakini kuna huyu uliyemtaja green water snake na boomslangs kiasi fulani wanafanana... Sasa ukikutana nae mara ya kwanza unaweza ukajichanganya... Na kujichanganya kwa boomslangs ni mwanzo wa kuandaa matanga... sababu Hakuna dawa ya kuondoa sumu ya boomslangs
 
Nipo naangalia kipindi cha Snake In The City hapa jamaa hao anawapapasa na mkono kama anachezea fimbo!

Ana hatari huyu!!!
 
Back
Top Bottom