Msaada: Huyu ni nyoka wa aina gani?

usiate tabu huyo ni nyoka wa kawaida sana ila tafuta matairi mengi choma moshi usambae puliza mafuta ya taa kwenye mashina ya miti usimwage puliza na bomba la kunyunyiza dawa maeneo yote yenye uficho washa matairi angalau mara tatu kwa wiki watapotea kabisa.....
 
Kuna kipindi nilikuwa napambano nao nyumbani kwa kuchoma matairi ya gari wakapotea ila juzi kati nimearifiwa kuwa wameua kadogo kaliingia sebuleni wakaua. Sasa niko njiani narudi nyumbani kuendeleza vita nao. Muhimu uwe unamwagwa oil chafu kwenye kila mahala unahisi uwepo wao ndio dawa ya kwanza
 
Mmeita mpaka zimamoto kumuua brown house snake! Angekua green mamba je ambaye akiingia bustanini haumuoni au black mamba mwenye Kasi
Mnaua tu ndio maana nature inawapiga na mavita,maradhi,matetemeko nk
Umenikumbusha mbali kidogo vita baina yangu na green mamba.
Oya green mamba hafi kizembe aisee.
 
Hapa nilipo kuna mzee anadawa za hawo viumbe na jins ya kuwaita na kuwauwa au kuwafuga kama hutojali nikuunganishe naye
 
Mwaga oil changanya na mafuta ya taa weka kwenye sehem unayohis nyoka wapo
Tumia njia za asili za kutengeneza Harufu itakayowaondoa hao viumbe eneo unaloishi.

Fyeka majani,fukia vishiml unavyoviona mazingira safi sio rafiki kwa nyoka.

ila ukiendelea ishi na vichaka,karibu utawaona sana wakija kufanya party hapo hapo home.
 
Hapa nilipo kuna mzee anadawa za hawo viumbe na jins ya kuwaita na kuwauwa au kuwafuga kama hutojali nikuunganishe naye
Acha uwongo bro kwamba Kuna dawa ya kuwaita?
Siku hizi watu wameelimika mganga
 
Tahadhari ni muhimu kwako kwa kipindi hiki na nyoka uliyemuua hana sumu na hata kama anayo hana sumu ya kutisha.

Na uli umtambue nyoka kama anasumu kali ni kutokana na rangi na meno yake kadri nyoka anavyokuwa mweusi au kijivu tiii ndivyo anavyokuwa na sumu kali,so huyo anasumu ndogo au hana kabisa.

Na wasikudanganye kwamba ni black mamba.Kwani black mamba huwa hawezi kabisa kukaa sehemu yenye kelele na kama angekuwa ndo yeye mmemuulia mtoto wake mwenye size kama hyo means yeye anaweza kuwa mara mbili ya huyo.

Basi hakika mpaka mda huu nyie ote mnaokaa hizo nyumba sijui hata kama mngekuwa mnaongea mpaka mda huu
 
Mafuta ya taa ni dawa kubwa sn ya kukimbiza nyoka, kingine ondoa vichaka vilivyo karibu na nyumba yako usafi ni muhimu sn huodoa hao viumbe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…