Msaada indicator ya gari ABS imewaka

Mkuu umejibu thread ya mwaka 2015[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]...nahisi jamaa hata hilo gari hana saa hizi!

Hajajibu kwa manufaa ya huyo muuliza swali tu....

Hii ni kwa ajili yetu sote humu jukwaani na yeyote mwenye fursa ya kupitia humu na ana miliki gari.....

Mimi nadhani katoa elimu nzuri sana kwa wote no matter mwanzisha hoja bado ana miliki gari hilo ama la....
 
mkuu ushauri wako sio mzuri sana kabisa.kwa Gari nyingine taa ya ABS ikiwaka shida huwa kubwa sana.na ukiendelea kuendesha unazidi kufanya uharibifu zaidi .kama kuharibu gearbox n.k

hasa huwa inategemeana ni aina gani ya gari
Yangu ni spacio inawaka tu sijui nayo ninini
 
Shida itakua sensors za kwenye maeneo ya matairi. Cha kufanya ifanyie diagnosis then ujue shida iko kwenye tairi gani. Hio sensor bi waya flani hv ambayo inaweza kua imechubuka ama imechomoka au imeisha. Pia tatizo linaweza kua associated na bearing. So njia bora ni kwenda garage wapate mengine zaidi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naomba ufafanuzi wa taa ya ABS Imewaka hata sijui gari ina shida gani. Nimejaribu kugoogle nimepata maelekezo ila nahitaji msaada wa watalaamu zaidi.

Nini madhara ya kuendesha gari taa ikiwa inawaka?
mfumo wa ABS unaosaidia unapokanyaga breaks yako, tyres zote kushika breaks kwa usawa na kiwango kimoja bila kuzidiana hivyo ukiendesha gari wakati mfumo ni mbovu ni hatari inapelekea gari kuteleza unapokanyaga breaks. Hivyo ni muhimu kurekebisha mfumo, Pia inapotokea dharura ukakanyaga breaks kwa nguvu na ghafla mfumo unakusaidia gari kusimama papo kwa papo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…