Ipi ni tiba sahihi kutibu tatizo la uume kelegea mbali na hizi dawa za asili zinazotrend sana mtandaoni?
Sent from my 23028RNCAG using
JamiiForums mobile app
Tiba ya uume kuwa imara ni mambo kadhaa:
1) Fanya mazoezi ambayo yatapelekea mzunguko wa damu kuwa wa kasi. Mazoezi kama kukimbia umbali mrefu, mazoezi ya kuruka kamba walau kwa takribani nusu saa hadi saa 1, Karate, Kucheza mpira n.k.
2) Jifunze kula vyakula halisi: Itambulike kwamba mazoezi huongeza hamu ya kula chakula chenye kuipa mwili nguvu. Hivyo, zingatia kula vyakula asili kama ni ugali kula ugali na mwanaume usile ugali umeregea au laini ugali mgumu ni muhimu sana. Na mara moja moja kula ugali wa mtama kwa samaki hapo utabamba😂😂😂.
3) Hakikisha uwe unakunywa maji ya kutosha walau lita 2-3 za maji kwa siku. Hii ni kwa sababu utakua unapoteza maji kupitia mazoezi unayofanya kwa njia ya jasho. Na hili ukiwa unafanya mazoezi utapenda kunywa maji mara kwa mara.😂😂
4) Jiepushe kuwa na msongo wa mawazo. Kama mwanaume inabidi utambue unajukumu la kukabiliana na kila tatizo hata likukute umelala inatakiwa upambane tu😂😂. Hivyo, ruhusu akili yako kuwa active wakati wote ili kukuruhusu kufanya hitaji lako la mwili.
5) Mwanaume epuke kunywa kunywa vinjwaji kama soda, pombe, uvutaji wa sigara, jamii ya juisi za mitaani usiyojua inatengenezwa vipi na jamii ya energy drinks. Kama kunywa kwa mwanaume, jitahidi walau kwa siku upate nusu glass ya wine. Wine huunguza mafuta mwilini.
6) Kua na mwanamke mwenye kujielewa, kuanzia usafi wa mwili, kinywa, mwenye kujua hali yako ya uchumi. Zingatia kua na mwanamke mmoja mwenye hizo sifa sio kua na kundi kubwa la wanawake hapo unajichimbia shimo.
7) Mwanaume jiepushe kwenda gym 😂😂😂 hapa wale wanaoenda gym watajua namaanisha nini.... Sitafafanua.
Fuata hayo utanishukuru baadae.