Msaada jamani afya yangu

Msaada jamani afya yangu

ethicx

JF-Expert Member
Joined
Apr 4, 2012
Posts
311
Reaction score
126
Habari wana JF jamani mimi nina sumbuliwa na tumbo sana huwa linajaa hata nikila kidogo, tumbo lina jaa gesi sipati choo vizuri maumivu ya kibofu yani tafrani nimejaribu kwenda hospitali nimeishia kupewa magnesium tu. Naombeni msaada wajuzi wa afya
 
Jaribu kutafuta aloevera gel ya kampun ya forever living uitumie,itakusaidia.naweza kukusaidia kuipata fungua kwenye google isome ukiridhika itafute.
 
Jaribu kutafuta aloevera gel ya kampun ya forever living uitumie,itakusaidia.naweza kukusaidia kuipata fungua kwenye google isome ukiridhika itafute.

Nme google maelezo yamenitosheleza kwahiyo ntaipataje na kwa bei gan?
 
kunywa maji mengi,na kula vyakula vyenye maji mengi,rudi kwa daktari bingwa,achana na uchafu wa alovera
 
Habari wana JF jamani mimi nina sumbuliwa na tumbo sana huwa linajaa hata nikila kidogo, tumbo lina jaa gesi sipati choo vizuri maumivu ya kibofu yani tafrani nimejaribu kwenda hospitali nimeishia kupewa magnesium tu. Naombeni msaada wajuzi wa afya
Mkuu ethicx Pole kwa kuumwa na tumbo jaribu dawa yangu huenda ikakusaidia inshallah..

KUONDOWA GESI TUMBONI:

TIBA 1:

Tayarisha vijiko vitatu vya unga wa Habat Soda,kijiko kimoja cha unga wa Mdalasini,kijiko kimoja cha Tangawizi ya unga,kijiko kimoja cha pilipili Manga,kijiko kimoja cha unga wa karafuu na kijiko kimoja cha kungu Manga.

Changanya vyote pamoja,utie maji kidogo kisha uchemshe kiasi.Kunywa ujazo wa kikombe kimoja cha kahawa (50ml) baada ya kula kutwa mara moja (1×1).


MARADHI YA KUFUNGA CHOO:


TIBA 1:SANAMAKI
Kwa mtu asiyepata choo kikubwa atachukua kiganja kimoja cha majani ya sanamaki ayachemshe mpaka yaive ili kipatikane kikombe kimoja cha chai (200ml).
Kunywa dawa hii kutwa mara moja (1×1).
Ikitokea haikufanya kazi baada ya masaa sita,basi mgonjwa ataongeza nyengine kama hiyo. Tumia kisha unipe Feedback.




Gesi kama ya Mtwara...I was kidding Mkuu MziziMkavu njoo huku utoe msaada tafadhali
Mkuu Petro E. Mselewa Vipi hali yako hujambo lakini? haya nimesha toa Tiba atumie kisha anipe feedback atapona inshallah.
 
Last edited by a moderator:
Ushauri wangu siyo kurudi kwa Daktari sbb alishakwenda na hakuna lolote alilosaidiwa. Ushauri wa REX ni mzuri sana auzingatie kwanza
 
Pole sana mkuu..
Uzoefu wangu umenionesha pia kunywa maji mengi ya vuguvugu asubuhi husaidia sana
jitahidi pia kula matunda aina walau 5 angalau mara 2 kwa siku..
 
Ndugu yangu itabidi ujieleze vizuri ili upate kusaidiwa. Dalili ulizotoa ni vague. Wazo linalogia ni kwamba Hunan hamu ya kula chakula ndiyo mañana ukila kidogo tu unajisikia kushiba. Pia usikula chakula cha kutosha huwezi kupata choo. Tafuta sababu ya kukosa hamu ya kula. Labda una stress ambayo inakuletea hali hiyo. Labda una minyoo au vitu vingi. Naomba utulie jaribu kujiridhisha na kula chakula ukipendacho. Kumbuka asilimia 40 ya magonjwa ya binadamu yanatibiwa kwa ushauri tu. naomba nikomee hapa kwa leo
 
Jaman asanteni sana kwa ushauri wenu nitafanyia kazi ushauri wenu.
 
Inawezekana pia ni dalili ya minyoo... mara ya mwisho ulikunywa dawa za minyoo lini?
 
Nmeanza kata tumbo kunywa maji ya uvuguvugu asubuh na kupunguza kula vyakula vya wanga nmeacha kunywa soda, sahv nakunywa maji mengi matunda kwa sana kimtindo choo napata vzur.
 
Inawezekana una Amoeba.

DALILI ZA AMOEBA:
1>Tumbo kujaa gesi.
2>TUmbo kuuma chin ya kitovu
3>Kujisaidia kinyesi cha kukatikakatika{kama kinyes cha mbuz}
4>Kujisaidia kinyes chenye kamasi.

TIBA:
>Nenda ukapime Amoeba hospitali na si kwingineko.
>Naamimini unaweza pewa METRONIDAZOLE Kama dawa na utapona kabisa.
>Usipende kula chakula kilichopoa hata kidogo.
 
Sanamaki ni majani gani hayo yanayoweza kusaidia kupata choo mkuu.Wenye matatizo kama hayo tupo wengi muheshimiwa.
 
Back
Top Bottom