Msaada jamani kwa mtu yeyote atakayetambua hii ndoto

UNAIJUA SADAKA YA LIMBUKO SAWASAWA?

LIMBUKO NI UZAO WA KWANZA, VYOTE VYA KWANZA NI VYA BWANA.

KWA MFANYABIASHARA: ATAPELEKA SADAKA YA FAIDA ALIYOPATA SIKU YA KWANZA ALIPOFUNGUA BIASHARA YAKE MPYA
KWA FAMILIA KAMA YANGU ZENYE MAFIRST BORN AMBAO KIBLIA NDIO LANGO LA FAMILIA TUNAPELEKA SADAKA KANISANI YA LIMBUKO KUMRUDISHIA BWANA VILIVYO VYAKE.

HUO MFANO NIMEUTOA WA AGANO LA KALE YES MUNGU ALIMJARIBU IBRAHIM ILA ALIMZUIA ALIPOJARIBU KUMCHINJA ISAKA AKAMWAMBIA AMTOLEE MWANAKONDOO ALIENONA.

HAPO UNAPOSEMA UJIMA SIJUI NANI KATI YETU AMBAE BADO YUPO KWENYE UJIMA
 
Ubarikiwe sana na YESU KRISTO aliye hai

Katika kitu ambacho walio wengi wanakosea ni kutokujua kuwa kila kilicho kizaliwa cha kwanza kwa binadamu, wanyama au mazao, nk...sio chako ni cha MUNGU muumba mbingu na nchi
 
Ubarikiwe sana na YESU KRISTO aliye hai

Katika kitu ambacho walio wengi wanakosea ni kutokujua kuwa kila kilicho kizaliwa cha kwanza kwa binadamu, wanyama au mazao, nk...sio chako ni cha MUNGU muumba mbingu na nchi
Amen🙏
 
Labda sijaelewa maana ya limbuko; hebu weka sawa basi, maana yake ni kumtoa huyo mtoto kafara au kuna mbadala? Niliposema ujima nilijua unamaanisha kutoa kafara. Kanusha kama sio kafara!
 
Unataka ushauri mkuu?au malumbano ya hoja au ujuaji wako wakati una tatizo?omba radhi.
 
Ndoto yeyoye unayoota kuanzia,
02 00 am to 04 00 am 99% ni uhalisia,
Na sio ya kupuuza.

Ndoto imelenga kukupa hasara inayohusu Mali zako au hasara inayohusu family yako.

Sababu mtoto umeokoa,,
Lakini nyumba imeteketea,

Means Kuna hasara kubwa ktk Mali zako inakuja,


Tafuta mtu wa Mungu akuombee,

Tunza comment yangu hii,
Utakuja kunikumbuka.
 
Mkuu ebu acha masihara Kama roho mbaya zishindwe kwa jina la yesu kristo
 
Ndoto ni ujumbe kwa njia ya roho kukupa taarifa ya mambo yajayo ama yaliyopita. Huenda kuna baya amefanyiwa mtoto wako ambaye hukuwaona na unapaswa kuwaokoa kiroho, mali kuteketea ni kukupa tahadhari uwe makini kwenye mambo yako usiwaze kupata tu chukua tahadhari na za kupoteza pia.

Punguza msaada omba kwa imani yako, fuata ushauri wa chumvi pia ogeshea watoto mara kwa mara, kumbuka wema hufa mapema.
 
Nyumba maana yake Ni wewe mwenyewe utapitia kipindi kigumu sana kiasi kwamba utapoteza pengine vitu vya thamani Ila Kama huyo mtoto ataugua atapona Ila Ni kwa kumhangaikia .
 
Asante
 
Nyumba maana yake Ni wewe mwenyewe utapitia kipindi kigumu sana kiasi kwamba utapoteza pengine vitu vya thamani Ila Kama huyo mtoto ataugua atapona Ila Ni kwa kumhangaikia .
Shukran mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…