TAARIFA KWA UMMA KUHUSU
UENDESHWAJI WA UDAHILI - ELIMU YA
JUU KWA MWAKA WA MASOMO
2012/2013
UTANGULIZI
Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (Tanzania
Commission for Universities-TCU)
ikishirikiana na Baraza laTaifa la Elimu ya
Ufundi (National Council for Technical
Education - NACTE) pamoja na Bodi ya
Mikopo ya Wanafunzi Elimu ya Juu (Higher
Education Students Loans Board)
inapenda kuutarifu umma kuhusu
utaratibu wa kujiunga na vyuo vya elimu
ya juu kwa mwaka wa masomo
2012/2013 kupitia mifumo ya Pre-
entry, Mature Age Entry, Equivalent
Qualifications na mfumo wa pamoja wa
udahili (Central Admission System) na
utaratibu wa mikopo kama ifuatavyo:
1. MFUMO WA UDAHILI KUANZIA
MWAKA 2012/13
1.1 Utaratibu wa Kuendesha Program za
Pre-entry na Mature Age Entry
Kuanzia mwaka huu 2012, vyuo vyote
vitakavyotaka kuendesha mafunzo ya
awali kabla ya mwombaji kustahili
kudahiliwa ili kuweza kujiunga na
programu za elimu ya juu (pre-entry
programmes) pamoja na kuendesha
mitihani ya kupitia mfumo wa Mature
Age Entry vinatakiwa kuwasilisha
programu hizo Tume ya Vyuo Vikuu (TCU)
au Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi
(NACTE) kwa uhakiki na kupata kibali.
Programu hizo ni lazima ziendeshwe kwa
muda wa mwaka mmoja. Hali kadhalika
kwa upande wa mitihani kupitia mfumo
wa mature entry, Tume kwa ushirikiano
na Baraza, kwa pamoja wataandaa na
kuratibu utaratibu wa mitihani katika
vituo maalum kikanda ili vyeti
vitakavyotolewa viwe na ulinganifu
unaostahili na hatimaye kuweza kutumika
katika udahili wa sifa linganishi katika
vyuo mbalimbali.
Vyuo vinatakiwa kuandaa programu za
mifumo ya Pre-entry na Mature Age
Entry na kuziwasilisha Tume na Baraza ili
zihakikiwe kwani mwaka wa masomo kwa
kusudi hili utaanza mwezi Agosti
2012/2013. Kwa utaratibu huu,
watakaofanya mafunzo hayo watatakiwa
kufanya mitihani yao na kujiunga na
masomo ya elimu ya juu katika mwaka wa
masomo 2013/2014.
Kwa taarifa hii, mwaka 2012/13
hakutakuwapo na udahili wa wanafunzi
kwa mfumo wa Pre-Entry na Mature
Age Entry.
1.2 Utaratibu wa Udahili Kupitia Mfumo
wa Pamoja (Central Admission System)
Waombaji watakaopitia mfumo wa pamoja
wa udahili (CAS) wamegawanyika katika
makundi manne, ambapo waombaji wa
kundi (i), (ii) na (iii) watatambuliwa kama
Direct Applicants na kundi (iv)
watatambuliwa kama Indirect
Applicants
(i) Waliohitimu elimu ya sekondari kidato
cha sita katika kipindi cha miaka miwili
iliyopita pamoja na wale watakaohitimu
mwaka huu.
(ii) Waliohitimu mafunzo ya diploma ya
elimu ya ufundi (NTA level 6) kutoka vyuo
vinavyotambulika na NACTE miaka miwili
iliyopita pamoja na wale watakaohitimu
mwaka huu;
(iii) Waliohitimu mafunzo ya Diploma ya
Ualimu (kutoka vyuo vinavyotambulika)
katika kipindi cha miaka miwili iliyopita
pamoja na wale watakaohitimu mwaka
huu.
(iv) Waombaji ambao sio wa moja kwa
moja (Indirect Applicants) ni wote
waliohitimu kidato cha sita, Diploma ya
Elimu ya Ufundi (NTA level 6) na Diploma
ya Ualimu katika kipindi cha zaidi ya miaka
miwili iliyopita (kuanzia 2009 kurudi
nyuma).
1.2 Waombaji Watakaowasilisha Maombi
yao Moja kwa Moja Vyuoni
Waombaji watakaowasilisha maombi
kupitia vyuo husika ni wenye sifa
linganishi (Equivalent Qualifications) yaani
wenye vyeti vya Astashahada na Diploma
ambazo hazitambuliwi moja kwa moja na
NACTE. Ili kukamilisha udahili,
wanashauriwa kuwasiliana na NACTE ili
vyeti vyao vitambuliwe na kusajiliwa kabla
udahili haujaanza.
Vyuo vinavyofundisha programu
mbalimbali katika ngazi ya Astashahada na
Diploma ambavyo havina usajili wa
NACTE/NECTA vinatakiwa kuwasilisha
matokeo ya wanafunzi wao NACTE haraka
iwezekanavyo ili matokeo hayo yaweze
kutumika katika utambuzi wa vyeti vya
wanafunzi husika.
2. MUDA WA UDAHILI KWA MAKUNDI
MBALIMBALI
Muda wa maombi wa kuwasilisha maombi
ya udahili kwenye CAS umegawanyika
katika makundi matatu kama ifuatavyo:
(i) Kundi la Kwanza (1 Aprili mpaka 30
Aprili 2012)
Waombaji wote waliomaliza kidato cha
sita, Diploma ya Elimu ya Ufundi (NTA
level 6), na Diploma ya Ualimu kuanzia
mwaka 2011 kurudi nyuma wataanza
kuomba udahili kuanzia Aprili 1, 2012 hadi
30 Aprili 2012.
(ii) Kundi la Pili
Waombaji wote watakaomaliza kidato cha
sita, Diploma ya Elimu ya Ufundi na
Diploma ya Ualimu mwaka 2012 wataanza
kuomba udahili baada ya matokeo yao ya
mitihani kutangazwa na vyombo husika.
Hakuna mwanafunzi atakayesajiliwa kwa
kutumia matokeo ya muda (provisional or
expected results).
(iii) Kundi la Tatu
Waombaji wote ambao ni raia wa Tanzania
waliosoma nje ya nchi au wenye vyeti
ambavyo si vya mfumo wa elimu ya
Tanzania (mfano: Cambridge,
Bacclaureate, n.k). Waombaji wa kundi hili
wanashauriwa kuomba udahili mara
matokeo yao yatakapotangazwa na
watatakiwa kupeleka vyeti vyao Baraza la
Taifa la Mitihani (National Examinations
Council of Tanzania NECTA) au Baraza la
Taifa la Elimu ya Ufundi (National Council
for Technical Education - NACTE) kwa ajili
ya kulinganisha alama zao za matokeo au
kupata ithibati kabla ya kuanza kuomba
udahili. Hakuna wanafunzi
watakaodahiliwa kwa matokeo ya muda.
3. UTARATIBU WA MIKOPO
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya
Juu kwa mamlaka iliyopewa kisheria itatoa
mwongozo na utaratibu wa utoaji wa
mikopo mwezi Februari 2012. Miongozo
hii itachapishwa katika vyombo vya habari
na kusambazwa kwenye vyuo vyote vya
elimu ya juu nchini na Ofisi za Posta na
kwa Wakuu wa Elimu kila wilaya. Maombi
ya mikopo kwa mwaka wa masomo
2011/2012 yataanza kupokelewa ifikapo
mwezi Machi 2012 na mwisho wa
kupokea maombi ni tarehe 30 Juni 2012.
Utaratibu huu utahusu waombaji wote
wapya na wale walioko masomoni katika
vyuo vya elimu ya juu.
4. HITIMISHO
Tunapenda kuwajulisha waombaji wote
kuzingatia muda wao wa udahili kama
ulivyoainishwa katika tangazo hili. Muda
ukiisha hawataweza kuomba hadi mwaka
wa masomo 2013/2014. Pia waombaji
wote wanashauriwa kufuata taratibu za
mikopo kam zitakazotolewa na Bodi ya
Mikopo ili kuepuka usumbufu unaoweza
kujitokeza katika swala hili
Maelezo zaidi na ufafanuzi kuhusu udahili
na mikopo wa 2012/13 yanapatikana
katika tovuti zifuatazo:
Tume ya Vyuo Vikuu; http://
Home - Tanzania Commission for Universities
Baraza la taifa la elimu ya ufundi; http://
NACTE : National Council for Technical Education | Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi
Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Elimu ya Juu;
Welcome to HESLB
IMETOLEWA NA: Katibu Mtendaji, Tume
ya Vyuo Vikuu Tanzania, S.L.B 6562, Dar
es Salaam. Barua pepe (e-mail)
es@tcu.go.tz
Attachment:
TUME_YA_VYUO_VIKUU_TANZANIA.pd