msaada jamani mtoto hachezi kama mwanzo

BLISS

Member
Joined
Mar 31, 2011
Posts
54
Reaction score
13
naombeni msaada nina wiki 15 ya ujauzito but mtoto hachezi kama mwanzo, nilipokuwa na wiki 7, na 8 ..yaani sasa huwa anajigusa mara moja kwa siku au 2, but nikisikiliza mapigo ya moyo huwa yanaenda kama mwanzo,,, na wala sina maumivu yoyote...naombeni ushauri jamani napata hofu..
 
Usiwe na wasi wasi hayo ni kawaida lakini cha muhimu nenda kamuone midwife au gynecologist hospitalini ambaye ataangalia mwenendo wa ukuaji wa mtoto.
 
Labda anaanza kutafakari misukosuko anayokaribia kuja kukumbana nayo kwenye huu uwanja wa fujo? LOL....
Nenda Hospitalini mkuu ili uweze kupata ufafanuzi wa kitaalamu... Hongera sana, nakutakia afya njema....
 
Usiogope hayo ni mabadiliko ambayo huwa yanatokea kwa mama mjamzito. Mtoto anaweza akacheza leo kesho asicheze. Au akacheza kwa mda halafu akatulia. Na hii inategemea mwili wako umeufanyisha kazi kwa mda mrefu sana bila kupumzika. Mama mjamzito anatakiwa afanye kaz lakin pia apate mda wa kupumzika.
 

Nadhani anawaza atakavyokumbana na nchi iliyokosa mwelekeo km bongo, jinsi gani atafika kwa babu Loliondo,na jinsi ya kuchoma moto magamba na vijusi vilivyojing'oa magamba.😛ound:
 
Hongera kwa kupata ujauzito.ila pole kwa kuwa na wasiwasi kwa hiyo hali,kwa kawaida hasa kwa ujauzito wa mara ya kwanza mtoto huanza kucheza week ya 16 hadi 20,lakini kwa ujauzito wa pili au zaidi huwahi week 2 au 3Kabla ya week ya 16 na kwa siku za kwanza huwa hawi active sana,kwa hiyo usiogope sana,ila ni vizuri ukimuona gynacologist
 

u mean alianza kucheza akiwa na 7 weeks?? Naona kama ni mapema sana kwa quickening kuanza,anyway upo mji gani labda nawrza kupa msaada wa dr mzuri kwa wanawake hasa wajawazito.
 
Dada wiki ya 7 sio mtoto huyo. Pia kuna scan hufanyika wiki ya 12 ulifanya? Hebu tumia internet kwa maswali yako hasa wakati huo uliopo.
 
Kabisa mkuu
umenena vema..
asante
 
Hamna mtoto wa wiki saba anayecheza ulikuwa unasikia vitu vingine.
Kucheza kunaanza wiki ya 16-20.
Subiria mateke yakija utayasikia na ndo utaamini uliyosikia wiki 7 haikuwa kitu.
 


Mhh! Wiki ya 7-8 alicheza? Nina mashaka!!! Anyway hebu jaribu kula vitu vitamu vitamu haswa Chocolate uone mziki wake!
 
ngoja nimuamshe jamaa tutengeneze batoto:mimba::mimba:
 
mhh! Wiki ya 7-8 alicheza? Nina mashaka!!! Anyway hebu jaribu kula vitu vitamu vitamu haswa chocolate uone mziki wake!

hata mimi nimeshtuka sana,c rahisi foetus acheze kwa muda huo. Ila inawezekana gas inamsumbua.
 
Haaaa kumbe una mimba! Hongera sana. Kwanini una wasiwasi kwani mpaka muda huu bado hujaanza kwenda kriniki? Kama unawasiwasi na afya yako njoo hapa Mwanza tunaye daktari bingwa wa akina mama na watoto.
 
nashukuru wote kwa msaada wenu... nitaufanyia kazi..
mlionipa hongera wote ..asanteni
ila siko karibu kwa huko mwanza..
mlioleta mzaa pia, mjaribu kutoa msaada na sio mzaa
hasa mtu anapokuwa na matatizo, coz
mzaa mzaa hutumbua usaha..
 
ni wakat wa ukuaji wa haraka wa mfumio wa faham so bada ana coordinate vizuri katika wiki hizo hapo
 
Mpigie ngoma atacheza.
Usijali mpenzi, atacheza tu, wiki 15 ni mapema sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…