Msaada jamani namna upimaji wa ultra sound unavyofanyika.

Mkwanda

Senior Member
Joined
Apr 6, 2012
Posts
122
Reaction score
14
Hivi karibuni nilikua nasumbuliwa na maumivu ya tumbo nikahisi naweza kua na uvimbe tumboni,nikaenda lugalo hosp wakanifanyia ultra sound kwa kuweka mashine chini kidogo ya kitovu then badae majibu yakasema sina tatizo.lakini namna ya upimaji ndio imenitia shaka coz mm nilizani mashine ingezungushwa tumbo lote lakini nimewekewa chini ya kitovu tu ndio imulike tumbo zima?wataalam plz!
 
Mkuu jinsia gani?

Kwa kawaida Ultrasound sonograph,(USS) hupima vitu mbali mbali (viungo vya mwilini, kutambua uvimbe(ulio na ile ambayo isiyo sehemu ya mwili) kwa kutumiamawimbi ya sauti.

Sasa upimaji hutegemea hasa jinsia, aina ya ultrasound, na kupima kuangalia kiungo/ viungo gani.
 
Nashukuru sana ndugu yangu,mimi ni mwanaume bt aina ya ultra sound siijui bt niliambiwa kabla yakupma lazma mkojo unibane sna ndio nipme, doct kaweka mafuta then akaweka mashne chini ya kitovu after 2mts tayar.bt mashne haikutembea tumbo zma.
 
Na mimi uncle wangu amepimwa juzi akakutwa na kokoto(gallstone) mbili tumboni.tumuombee apone wana jf
 
Nashukuru sana ndugu yangu,mimi ni mwanaume bt aina ya ultra sound siijui bt niliambiwa kabla yakupma lazma mkojo unibane sna ndio nipme, doct kaweka mafuta then akaweka mashne chini ya kitovu after 2mts tayar.bt mashne haikutembea tumbo zma.

Natumaini uliambiwa kunywa maji mengi,, mkuu pamoja na kuambiwa hivyo..nadhani sonographer alifuata maelekezo ya daktatri mf.
Kupimwa hapo/sehemu hiyo na kufuata masharti hayo, mostl likely ilikuwa kutathimini kibofu cha mkojo na enwo kuziunguka..iwapo kuna vipimo zaidi, au kulikuwa na umuhimu wa kupima tumbo la nyuma(mgongoni) mfano kutathimini figo, bandama n.k ingefanywa hivyo.

Hivyo nadhani ungeondoa shaka ya kutopimwa kote (yaani kuzunguka tumbo) kama hakukuwa na haja hiyo.
 
Nashukuru sana mkuu,Mungu akubariki.
 
Ultrasound ndo inavyopimwa. Mafuta yanapakwa sehemu tu husika na picha inapigwa kwa kutumia mawimbi ya sauti. Usiwe na shaka, shukuru Mungu tatizo lililohisiwa halipo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…