Swali: Ufanyeje ili uweze kuacha?
Jibu: 1. Dhamiria KUACHA kwa ridhaa yako mwenyewe na huku ukijiepusha na marafiki, shughuli na vyovyote vinavyohusiana na huo mchezo hata ushauri usitoe kwa mtu yeyote.
2. Jiambie kwamba unaweza hasa kwa kujikita katika shughuli zingine na hasa za kijamii, mazoezi au kujitolea huku ukijiepusha na matumizi mabaya ya fedha ya thamani yeyote ile na kama ni ngumu basi hakikisha unaandika matumizi ya fedha zako zote za kila siku hata iwe Tshs. 1 kwenye kijitabu kidogo kwa ajili ya kumbukumbu na hutajutia, sababu utajionea aibu na huruma pia.
3. Fanya Kazi, Fanya Kazi na mwishowe Uchape Kazi kwa Nguvu zote.(Kinachoingia kwa Jasho, Kitatoka kwa Jasho)
JITAHIDI UNAWEZA.