Msaada jamani. Natafuta vyeti.

mbalisana

Member
Joined
Dec 15, 2011
Posts
46
Reaction score
42
Nilipotelewa na vyeti vya shule. Olevel na Alevel. Nimejaribu kuvitafuta nileenda TCU nikaangalia database ya wanafunzi walioenda vyuo vya elimu ya juu,nikidhani huyu aliyevichukua kaamua kuvitumia sikufanikiwa. Natamani nipate vyeti vyangu, napata shida sana ninapoomba kazi hawataki statement of results wala results slip. Naomba kujua kama kuna njia ambayo naweza kutumia kutafuta mtu anayetumia vyeti vyangu. Maana viliibiwa inasemekana na mwanachuo mwenzangu nikiwa chuo ushahidi ulikuwa mdogo sana hivyo sikupenda kusababisha ugomvi. Bado navitafuta.
 
Dah!pole sana mkuu,vilipotelea wapi na mwaka gani?
 
Hata ukimpata unadhani atakurudishia kwenye bahasha?
Kuna utaratibu wa jinsi ya kupata msaada unapoibiwa vyeti. Nenda baraza la mitihani watakuelewesha. Lakini kwanza tafuta police report kuwa umeibiwa. Baada ya hapo utaratibu; endapo haujabadilika; unapaswa kutoa tangazo kwenye gazeti la serikali (wanajua wenyewe jinsi ya kuandika). Baada ya siku 21 unaweza kuomba matokeo yako kwa ajili ya kila application unayofanya. Namaanisha kila unapohitaji cheti, baraza la mitihani wanamuandikia uneyempelekea barua ya matokeo.
 
Hii imeka vyema sana hakuna njia nyingine.
 
Oya,kuna vyeti viliokotwa vikawekwa pale daruso-udsm,{vipo mpaka leo}inasemakana vina zaidi ya miaka mitatu pale,asa sijui ndo vitakua hvo au vp?kipo kimoja cha o-level na results slip ya form 6.
 

huo utaratibu nimeshautumia mara nyingi. Baraza wanato statement of results ambayo bado sehemu nyingi ni tatizo. Na matangazo mengi ya kuitwa kwenye usahili wanasema hawataki statement of results.
 
Oya,kuna vyeti viliokotwa vikawekwa pale daruso-udsm,{vipo mpaka leo}inasemakana vina zaidi ya miaka mitatu pale,asa sijui ndo vitakua hvo au vp?kipo kimoja cha o-level na results slip ya form 6.

shukrani sana. Nitaenda niulize. Ingawa vyangu vyote vilikuwa ni vyeti. Labda vipo vingi.
 
Pole sana, kwa ninavyofaham necta hawatoi cheti zaidi ya mara moja na kwa bahati mbaya sana ikitokea ukapoteza cheti (cha NECTA) ujiandae kua rafiki wa NECTA maana kila mara uhitajipo kitu kihusianacho na cheti/vyeti chako/vyako lazima uende pale barazani wakutengenezee statement kama ulivosema hapo juu.

Kiukweli hakuna namna rahisi ya kupata hivyo vyeti vyako ila kama kwenye interview hawataki statement usiwe unakata tamaa, jaribu kua unawaelewesha wakigoma basi hakuna namna.

Zaidi ya hapo labda tuombe NECTA wafanye mabadiliko ili wawe wanaendelea kutoa vyeti zaidi ya mara moja pale inapothibitika cheti/vyeti kupotea. Kwa nyongeza labda kuwe na mfumo wa kuvibatilisha vyeti vinavyosemekana kupotea ili kuweza kutengeza vingine na jambo hili liendane na teknolojia ya kuweka mfumo wa kielektroniki kwenye cheti badala ya ile hologram.

Asante, haya ndiyo mawazo yangu.
 
Mungu akusaidie mkuu upate vyeti vyako and hope utavipata tu maana ni haki yako.
 
Mie inanigharimu kama ww cheti changu O-Lvl kilipotea ..tuwaombe NECTA waangalie namna nyingne kwani watu wengi wanaumia
 
Pole sana mkuu,mi mwenyewe ni mhanga nilipoteza kuanzia cha o'level mpaka cha chuo,nimetoa taarifa polisi wameshindwa kunisaidia hata baada ya kuwapa simu ya mtu aliyenipigia na kudai anavyo na baadae kupotea hewani kabisa. Natamani NECTA wangebadili utaratibu wao kwa waliopoteza vyeti!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…