Abbasfarudume
JF-Expert Member
- Feb 14, 2017
- 1,625
- 1,326
Natafuta mwanasheria wa kunisaidia nataka kuwafungulia kesi ya madai tigo wanilipe fidia million mia mbili kwa kunisababishia Usumbufu. Ni hivi ilikuwa Jumapili ya tarehe 12 mwezi huu wa tisa 2017 majira ya saa tano na dakika 16 hivi au 17. Nilienda kufanya muamala wa kutoa pesa kwa wakala wa tigopesa kiasi cha jumla cha pesa 48500 hili nitoe pesa ya matumizi nyumbani kwa bahati mbaya. Nikakosea kutuma namba ya wakala, wakala niliemtarajia kumtumia pesa anaitwa Emmanuel semamba mwenye namba ya uwakala 15182. Sasa mimi kwa makosa ya kibinadamu nikatuma ile namba ya wakala kwa bahati mbaya nikamtumia wakala anaenda kwa jina la hemed shaban. Sasa kwa muda huo na saa hizo hizo ikabidi niwapigie tigo idara ya huduma kwa wateja wa tigopesa. Nikawaeleza tatizo langu wakaniambia kweli wameona tatizo langu lkn nisubiri ndani ya masaa 24 tatizo langu wanalishughulikia kwa hiyo ikawa sina budi kuvuta subra kwa muda huo wa masaa 24 kuwavutia subra na hiyo ndio ilikuwa hela ya chakula na mahitaji mengine madogo madogo ya kuwa achia familia yangu pale nyumbani kwa siku hiyo. Basi kila nikiwapigia madai kwa upande wa kwao ayaishi mara system ya mfumo wa tigopesa mbovu mara madai yako yamepelekwa kitengo maalum subiria ndani ya masaa 24 utapata pesa zako mara subiri ndani ya masaa matatu alafu piga utapata pesa zako mara subiria ndani ya masaa 12 utapata pesa zako. Yaani wananisaundisha tu sasa mimi nimeshachoka naombeni msaada na Ushauri nataka kuwashitaki hii kampuni inilipe Fidia million mia mbili. Tahadhari natoa Majibu ya karaha na kashifa sitaki kama huna majibu pita tu waache wengine wenye kujielewa Wajibu na kunipa Mawazo na Ushauri Povu sitaki karibuni sana wana jukwaa kwa sababu leo kwangu Kesho kwa mwingine jambo kama hili linaweza kumfika na kumkuta!