Msaada jamani

Msaada jamani

Tutor B

JF-Expert Member
Joined
Jun 11, 2011
Posts
9,025
Reaction score
6,598
Aliwahi kuolewa kwenye familia ya waarabu akaachika kwasababu hazai. Nilipokutana naye kwa mara ya kwanza ukweli huo hakunieleza.Niliendelea naye hadi akapata ujauzitona kujifungua mtoto wa kiume ambayeanapendeka sana ujombani kwao. (Usiulizeni kwa nini sijampeleka nyumbani kwetu)
Tatizo: Anadai siku hizi akilala bila kupata hata bia mbilindoto zake ni kuwaota waarabu akiwa nao sehemu ambayo hajui.
Jingine: Ikitokea nikatoka naye out hata pesa ningeilindavipi inapotea. Na yeye hana tabia ya udokozi. Nifanyeje, kuna aliyewahikukutana na tatizo la namna hii? Nisaidieni ushauri.
Aliwahi kuolewa kwenye familia ya waarabu akaachika kwa sababu hazai. Nilipokutana naye kwa mara ya kwanza ukweli huo hakunieleza. Niliendelea naye hadi akapata ujauzito na kujifungua mtoto wa kiume ambaye anapendeka sana ujombani kwao. (Usiulize ni kwa nini sijampeleka nyumbani kwetu)
Tatizo: Anadai siku hizi akilala bila kupata hata bia mbili ndoto zake ni kuwaota waarabu akiwa nao sehemu ambayo hajui.
Jingine: Ikitokea nikatoka naye out hata pesa ningeilinda vipi inapotea. Na yeye hana tabia ya udokozi. Nifanyeje, kuna aliyewahi kukutana na tatizo la namna hii? Nisaidieni ushauri.
 
Mmh waarabu wanafanya mambo! Maombi ndo solution pekee!
 
Mmh waarabu wanafanya mambo! Maombi ndo solution pekee!
Asante kwa ushauri wako; japo nawaza kumtosa kama mwalabu alivyomtosa kwa kutopata mtoto, mimi namtosa kwa mauzauza yake hayo! Au wasemaje?
 
Nenda mkaombewe na muoche kufikiria fikira hizo just ignore yatakwisha
 
Nenda kanisani ukafanyiwe maombi!
 
ana mapepo huyo, nenda mkafanyiwe maombi!!!!!!!

Unasemaje kuhusu dawa ya moto ni moto. Kama ana pepo kwanini nisimpeleke kwenye wataalam wa mapepo tofauti na makanisani.
 
Unasemaje kuhusu dawa ya moto ni moto. Kama ana pepo kwanini nisimpeleke kwenye wataalam wa mapepo tofauti na makanisani.

mule mule tu....
dawa mpeleke baharini muda wa saa za jioni....
 
Back
Top Bottom