Msaada: Je, nifanye nini ili niweze kupata pesa ya kujiajiri?

Professional Trader

JF-Expert Member
Joined
Apr 5, 2016
Posts
1,220
Reaction score
1,120
Mimi ni muhitimu wa chuo kimoja wapo apa nnchini katika ngazi ya diploma, nilikua nawishi siku moja niwe moja kati ya wajasilia mali wakubwa apa nchini ila tu Tatizo linakuja pindi tunapofikia kwenye swala la MTAJI na ukizingatia ndo nimehitimu chuo kama wiki mbili nyuma yani apa mtaji nilio nao sahivi ni vyeti vyangu tu .

Lengo la kuandika hii post ni kuomba msaada kama kutakua kunanjia mbarimbari ambazo naweza Fanya ili kupata mtaji pesa ambao ndo muhimu zaid ingekua vizuri mkanisaidia ndugu zangu au hata kma ikitokea kuna nafasi ya kazi flani pia nikaifanya sio mbaya ili tu na Mimi siku moja nifike sehemu flani na ikiwezekana nisaidie watu wengine wataokuwa wakiitaji msahada mka ilivyo mimi leo hii
 
.rekebisha hilo neno kwenye "heading"ili tujue unahitaji nini.
 
Mtaji unawezakuwa ujuzi uliosomea kipaji ulicho nacho ama kuwa mshauri wa kulipwa katika fani uliosomewa inaweza kukusaidia kukupatia mtaji na ukagrow.
 
Kijana mtaji sio tatizi tatizo unataka kufanya nini. Unataka.kuwa mfanya biashara mkubwa,je unawazo linalotekelezeka? Au ndio ile ya kusema nikipata hizo.pesa sitokosa cha kufanya mwisho wa.siku unaishie kununua smart phones.za.bei ya juu na smart sscreen basi.
 
Umekosea kujenga hoja. Ungekuja na biashara uombe mtu wa kuifadhili mgawane faida. Hata benki zinafadhili wazo zuri la biashara.
 
Kama wadau waliyotangulia hapo juu tatizo tulilonalo wengi ni wazo zuri la biashara linalotekelezeka NA sio mtaji kama wengi tunavyofikir hivyo bas pengine ungeweka wazo lako ili wajumbe wakuchangie mawazo.
 
Umekosea kujenga hoja. Ungekuja na biashara uombe mtu wa kuifadhili mgawane faida. Hata benki zinafadhili wazo zuri la biashara.
Mkuu umetoa ushauri mzuri sana hadi umenivtia 7bu i have the same case. Wazo langu ni kuanzisha SalaryPay-hii ni mobile money app of phones ambyo itawasaidia makampn binafs na serkl kulipa mishahara ya wafanyakaz wao kuptia simu bila kuwa na bank acc hvy natafuta mfadhili amby ntampa hisa ktk mradi.
 
Okay nimewaelewa ndugu zangu na naufanyia kazi ushauri wenu najiandaa kuleta moja ya mpango wangu wa biashara ambao hauitaji kiasi kikubwa sana cha pesa na natumai ni dili sana asa kwa hii location niliyoitageti kutokana na demand yenyewe ya wahusika wa hapa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…