Ni mwaka wa 10 Sasa ni kwamba nimeshindwa! Kwani nimekuwa mtaratibu sana kwao. Hatua ya kwanza nimekuwa nikiwaelimisha Kwa muda mrefu lakini wanajifanya hawaelewi. Pia nimeshafika hadi ofisi ya Kijiji na waliitwa na wakapuuza. Police nilishafika lakini sikupata msaada. Pia katika kuwaelimisha nimekuwa nawaeleza jinsi wanavyonidumaza kiuchumi maana sifanyi maendeleo yoyote wakati Mimi maisha yangu yanategemea Shamba, lakini wao ng'ombe zao zinazidi kuzaliana kwa kutegemea Shamba langu. Sina faida kwani ata shilingi sipati zaidi ya kunidharau tu. In
Naona Sasa ifike mwisho kwani sioni faida ya Kuwa na shamba, Ina maana Mali yangu initese mwenyewe, haiwezekani! Wanajifanya watemi kwenye Mali za wenzao. Suluhisho pekee la mwisho ni kuuchukua ushauri wa member aliyetangulia hapo juu wa kumwaga mboga!! Ndio mboga tu ndani ya eneo langu ninalolimiliki kihalali, kwani wao wanamwaga ugali! kwani Kuna wakati nilishawahi kuwataharifu Kwa maandishi kuwa wasichunge ktk eneo langu kwani nataka kulima Kwa kukausha majani Kwa sumu lakini wakapuuza, sijui wanategemea miziziology! Au wanaona nawaogopa! Sasa naona nitafanya kweli. Cha muhimu Bado naangalia kisheria zaidi kama Kuna Sheria' yoyote inayonizuia kufanya lolote ndani ya eneo ninalolimiliki kihalali.
Sent from my Infinix X6512 using
JamiiForums mobile app