silent lion
JF-Expert Member
- Feb 28, 2012
- 1,278
- 1,794
Wadau habari za jioni. Mida hii wakati natokea sehemu fulani kuelekea nyumbani, nilipishana king'ora cha polisi kuashiria kua kuna msafara wa kiongozi wa nchi anakuja. Hivyo nikakaa pembeni nikazima taa za gari ili kupisha msafara. Mara msafara ukawa unakaribia, kwa wingi wa magari na vimulimuli nikajua ni Mheshimiwa Rais wa Zanzibar, hivyo nikaendelea kukaa pembeni kumsubiri apite. Lakini kwa vile njia yenyewe aliyokuwa akipita ni nyembamba na ilikuwa kiza kwa kukosekana taa za barabarani, nikaona ni heri niwashe taa zangu nilizokuwa nimezizima ili ule msafara usike ukanivaa ukizingatia kuna magari yanakuwa yanatanua. Cha kustaajabisha askari aliyekua katika king'ora cha mbele kabisa akanitolea lugha chafu kwa kuniita --------, sasa ndo mpaka sasa nimepigwa na butwaa kosa langu ni lipi, labda wadau wa JF mnaweza kunielekeza ili siku ya pili nisirejee tena. ahsanteni