Msaada: Jee hili ni kosa kisheria?

Msaada: Jee hili ni kosa kisheria?

silent lion

JF-Expert Member
Joined
Feb 28, 2012
Posts
1,278
Reaction score
1,794
Wadau habari za jioni. Mida hii wakati natokea sehemu fulani kuelekea nyumbani, nilipishana king'ora cha polisi kuashiria kua kuna msafara wa kiongozi wa nchi anakuja. Hivyo nikakaa pembeni nikazima taa za gari ili kupisha msafara. Mara msafara ukawa unakaribia, kwa wingi wa magari na vimulimuli nikajua ni Mheshimiwa Rais wa Zanzibar, hivyo nikaendelea kukaa pembeni kumsubiri apite. Lakini kwa vile njia yenyewe aliyokuwa akipita ni nyembamba na ilikuwa kiza kwa kukosekana taa za barabarani, nikaona ni heri niwashe taa zangu nilizokuwa nimezizima ili ule msafara usike ukanivaa ukizingatia kuna magari yanakuwa yanatanua. Cha kustaajabisha askari aliyekua katika king'ora cha mbele kabisa akanitolea lugha chafu kwa kuniita --------, sasa ndo mpaka sasa nimepigwa na butwaa kosa langu ni lipi, labda wadau wa JF mnaweza kunielekeza ili siku ya pili nisirejee tena. ahsanteni
 
Kwenye jukwaa la sheria kule mkuu ungepata wachangiaji wengi zaidi ya huku.
 
Pole sana mkuu. Mimi si mtaalamu wa sheria, lakini kwa ufahamu wangu hukufanya kosa kuwasha taa, hasa ukizingatia kulikuwa na giza na 'poor visibility', ambayo ingeweza kuleta madhara kwako wewe na hata kwa hao waliokuwa kwenye msafara. Tusubiri wataalamu huenda watatufafanulia zaidi!
 
Mkuu huo msafara ulikuwa unatoka unakokwenda au ulikuwa unakwenda unakokwenda?

Kwa kusema hivyo labda taa zako ziliwapiga usoni, pia lazima uliwashtua wakadhani unataka kuingia barabarani,

Nadhani unakumbuka kifo cha Sokoine kilitokeaje
 
Mkuu huo msafara ulikuwa unatoka unakokwenda au ulikuwa unakwenda unakokwenda?

Kwa kusema hivyo labda taa zako ziliwapiga usoni, pia lazima uliwashtua wakadhani unataka kuingia barabarani,

Nadhani unakumbuka kifo cha Sokoine kilitokeaje

msafara ulikuwa unatoka ninakokwenda, sokoine ilikuwaje kwani?
 
Hao ndo askari wetu bwana, wamezee tu.
 
pole mkuu ila inategemea na ukali wa taa zako za gari, kwa ufahamu wangu mdogo nadhani kuwasha taa ghafla kungeweza kumpofusha dereva wa msafara na kusababisha ajali, ulikua na nia njema ila muda haukua muafaka, ungewasha zile za chini ama indiketa, kusudio likiwa kuwajulisha kua umepaki, au taa nyingine yoyote zisizo na mwanga mkali, pole sana..unabahati wali kutusi tu ingawa haikuwa sahihi, ungeingia kwenye matatizo makubwa kama lingetokea la kutokea kwa bahati mbaya...
 
at least am still in one piece, thanks to the lord for that.
 
Pole kwa yaliyokusibu ila kama kwer ni dereva kuna temporary packing ndizo ulizotakiwa kuwasha na si zinginezo sasa sijajua uliwasha taa gan mkuu
 
Huyo askari alikuwa na stress zake tu. Asikupe mawazo. Huna kosa hapo. Poleee
 
Inategemea uliwasha taa gani deamlight au full light, lakini kama ni deam light ulikuwa sahihi ili uweze kuonekana. After all hawa askari wetu hawajui sheria kwa hiyo si kosa lao. Mfano hawajui kwamba kuwasha taa mchana si kosa wao watakwambia ni kosa lakini halipo kwenye sheria zetu
 
Back
Top Bottom