Msaada:jini mahaba lilitaka kunibaka!!

manyata

Member
Joined
Mar 26, 2013
Posts
41
Reaction score
6
Hallow,wana JF,

Kuna kisa kimenikuta juzi kati.Mimi ni mwanaume miaka 40.

Wakati nikiwa usingizini nikawa kama naota hivi na pembeni akawa yupo binti mrembo mzuri na mrefu kiasi.

Ghafla akanikumbatia na kuanza kunipet pet,kama vile ni binti wa kweli.wakati huo nguvu zilikuwa zimeniishia lakini nilibahatika tu kukemea kwa jina la YESU,likawa linasogea na kadri nilivyokemea likawa linasepa hadi naliona hilo linasepa kwa dirishani ingawa lilikuwa limefungwa.

Naomba kujua ndugu zangu,hii imekaaje?maana nasikia kuna Majini yanazini na binadamu.nini madhara yake kama ikikutokea? Tiba ya hii ni nini?
Ahsanteni
 
Kemea kwa jina la YESU mapepo,majini na roho mbaya zisikufwate..polee
 
Kama hujaoa kaa karibu sana na MUNGU wako manaake hayo majini yaweza kuwa yanafukuza wachumba zako kwa kukufanya uonekane na matatizo au wewe uwaone wao hawafai na kama uko kwenye yanaweza kukuletea mtafaruku ili ndoa ivunjike kama kuharibu mimba na mengineyo.
 
Ulijuaje kama hilo lilikuwa jini mahaba? Litake halafu liache? Nafikiri unasikia tu madudu hayo wewe!
 
kwa ninvyoelewa Majini Mahaba yapo na huwa na uhusiano na wanadamu katika ulimwengu wa kiroho, unaweza hata kuwa na familia katika ulimwengu wa kiroho... km Bible inavosema.. kazi ya shetani ni kuchinja na kuharibu na hapana uhusiano kati ya nuru na giza, mapepo yapo katika ulimwengu wa giza japo yana uwezo wa kijidhiirisha katika mwili maana wao ni roho, kuwa makini ndugu yangu na umtafute Mungu mana hayo yanaharibu tu, yanaweza kuharibu maswala yako ya ndoa, unaweza usipate watoto na tatizo ukitafuta hospitali hakuna, wakati mwingine yanaingia mpka kwenye your finances, na kama hujao wala kuolewa hawawezi kukubali tena uoe binadamu so ni shida tupu...unatakiwa kusali na kijikinga na ukigo wa Mungu
 

kweli kabisa, mambo haya yalishanipata.
 
siumesema ukikua unaota? au /????????????????????????????? NINI MAANA YA NDOTO...
mwenzako hua naota napokea mahela mengi natulia tu sikemei wala nini still siyaoni kumbe ndoto
 
Mkuu umeulizia dawa wkt umeshaitumia tayari? Ulimtaja yesu jini likatoka maanake ndo dawa hiyo
 
Ni kweli hilo ni jini, azma yake kuu ni kukutenga na nguvu za Mungu,
Na kukuharibia mambo yako na mahusiano yako
Funga na kuomba
 
Hongera kwa kupona kwenye mbako
haaaaaa... ningekuwa mimi nisingeleta purukushani ningetulia tuli kama maji yamtungini!! yani mwanamke aje kunibaka nipige kelele a we naanzajeanzaje kwamfano😀
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…