Msaada: Jinsi kutengeneza Mandazi

Msaada: Jinsi kutengeneza Mandazi

babu M

JF-Expert Member
Joined
Mar 4, 2010
Posts
5,222
Reaction score
3,173
Naomba msaada jinsi ya kutengeneza mandazi ya kumimina(sina uhakika na jina)
Huku nilipo sasa hivi vitafunio ni Toast,bacon,sausage and baked beans(english breakfast), hii imenishinda na Mcdonalds b'fast zao zimenitoka sasa hivi.

Ni unga gani ninatakiwa nitumie, self raising or plain? na jinsi ya kuchanganya.
 
hee na mie nasubiria nione hizo recipes...

nadhani wale akina bitimkongwe watakuwa wanajua haya!

lingeazishwa jukwaa la mapishi humu jamii forums,tuwe tunapeana maujuzi eti eeh?
 
Ni kweli kabisa, imenichukuwa muda kuangalia sehemu gani nianzishe hii thread. Inabidi tumwombe invisible aliangalie hili jambo.

Watu wengine tumekuwa mara nyingi tuko nje ya Tanzania,baada ya muda unaanza ku-miss vyakula ulivyo vizoea na haujuwi jinsi ya kuvitengeneza kwasababu nyumbani ulikuwa una nunua ama unatengenezewa.

Pia kwa wale walioko nyumbani itawasaidia badala ya kwenda kumgongea jirani au kuchuwa maelezo kwenye simu ambayo ni garama kubwa.
 
Mkuu, kuna tofauti kati ya maandazi, vitumbua na mkate wa kumimina. Maandazi yanapikwa kwa kutumia unga wa ngano wakati vitumbua na mkate wa kumimina vinapikwa kwa kutumia unga wa mchele. Tofauti ya mkate wa kumimina na vitumbua hasa ni size, mkate mkubwa na vitumbua size ya cup cake.

Unga wa self raising una chumvi na huhitaji hamira unapika papo kwa papo, unga plain utahitaji hamira, na ukishandaa utangojea uumuke ndio upike, huu ndio unatumiwa na wengi. Hopeful utapata recipes, akina sie tumejifundisha kwa kuangalia na tunarekebisha as we go!
 
nadhani huyu anahitaji kujua jinsi ya kutengeneza kaimati au kalimati kama sikosei. mwenye kufahamu jinsi ya kuzitengeneza hizi plz atuwekee
 
img_0050.jpg

DES-BananaBeignets.jpg

Labda Picha itanisaidia kueleweka zaidi since im not sure with the name.
Ninayotafuta recipe nje yanafanana kama hayo kwenye picha tofauti hayo hapo juu ndani yako kama doughnut na ninayotaka ndani ni malaini.
 
babu M nimeshindwa kujua kama haya yako ni maandazi ya mafuta ( au wengine wanaita maandazi ya kuchoma) au ni kaimati au ni badia (badja) au vikhosa ( au wengine wanaita vilosa)

kaimati na vilosa vinapikwa ikisha vinamwagiwa shira kwa juu ( yaani ukivitumbua vinatoka sukari kwa ndani)

badia zinatengenezwa kwa unga wa dengu (nitaweza kukupa recipe kama ukitaka)

kwa kuwa umeyaita maandazi nafikiri itakuwa ni hayo ya kuchoma
haya yako ya aina mbili .......
watu wa bara wengi wanafanya yanakuwa magumu hivi kwa mfano wa kama half cake hivi (hard na ndani iko kavu) ambayo yanatiwa baking powder na sio hamira
watu wa pwani wao wanafanya yanakuwa malaini ( ukiyabonyeza yanabonyea hadi ndani) na yanatiwa hamira na sio baing powder.

Ukishaamua unapenda yepi kati ya hayo tunaweza kukupatia recipe .......
 
Asante kwa msaada wako.Ninatafuta hayo kwenye nyekundu...Nimejaribu ku-google websites nyingi wameweka hayo ya baking powder lakini ya hamira nimeshindwa kupata kabisa.Ninataka ndani yawe malaini kabisa
 
hiyo link uliyopewa Maandazi | Alhidaaya.com ndio inaonyesha maandazi hayo ya kubonyea mpaka ndani .......kama wenye recipe zake ilivyoandikwa unatia hamira na sie baking powder.

nadhani ukifata maelezo kwenye hiyo link utafanikiwa......( picha zake pia ziko clear step by step utafika tu)
 
Hie all JF?
My friend is in need of a house or an apartment for rent

Descriptions:-
With master and two other bedrooms excluding kitchen facility and public latrine
At least one car parking space and fence preferred
must be at standard area,not too rural oriented,easily reachable with source of water and sewage disposal system.

Locations:
Cinza,mwenge,magomeni,along kawawa road,near places of mbezi(hates heavy traffic) and similar places(near the city)

Price- up to Tsh 300,000 x12

When required at anytime before 28/8/2010

Any person with information, please let me know but I don't prefer "dalali"
pm
My kind regards in advance

N:B I COULD NOT POST AS FRESH THREAD AS PEOPLE ARE BUSY COOKING
 
hee na mie nasubiria nione hizo recipes...

nadhani wale akina bitimkongwe watakuwa wanajua haya!

lingeazishwa jukwaa la mapishi humu jamii forums,tuwe tunapeana maujuzi eti eeh?

Miye miaka ya nyuma nimeshaomba sana jukwaa la mapishi hapa bila mafanikio. Babu M hizo naona kama ni kalimati na si maandazi.
 
Naomba msaada jinsi ya kutengeneza mandazi ya kumimina(sina uhakika na jina)
Huku nilipo sasa hivi vitafunio ni Toast,bacon,sausage and baked beans(english breakfast), hii imenishinda na Mcdonalds b'fast zao zimenitoka sasa hivi.

Ni unga gani ninatakiwa nitumie, self raising or plain? na jinsi ya kuchanganya.

Bofya hapa
 
hiyo link uliyopewa Maandazi | Alhidaaya.com ndio inaonyesha maandazi hayo ya kubonyea mpaka ndani .......kama wenye recipe zake ilivyoandikwa unatia hamira na sie baking powder.

nadhani ukifata maelezo kwenye hiyo link utafanikiwa......( picha zake pia ziko clear step by step utafika tu)
Nilishapita huko lakini sikuona kitu.
 
Hie all JF?
My friend is in need of a house or an apartment for rent

Descriptions:-
With master and two other bedrooms excluding kitchen facility and public latrine
At least one car parking space and fence preferred
must be at standard area,not too rural oriented,easily reachable with source of water and sewage disposal system.

Locations:
Cinza,mwenge,magomeni,along kawawa road,near places of mbezi(hates heavy traffic) and similar places(near the city)

Price- up to Tsh 300,000 x12

When required at anytime before 28/8/2010

Any person with information, please let me know but I don't prefer "dalali"
pm
My kind regards in advance

N:B I COULD NOT POST AS FRESH THREAD AS PEOPLE ARE BUSY COOKING
Don't you think it's rude to place your ad to someone else thread?
 
Miye miaka ya nyuma nimeshaomba sana jukwaa la mapishi hapa bila mafanikio. Babu M hizo naona kama ni kalimati na si maandazi.
Ninayo tafuta hayako coated na sugar or syrup outside, yapo kama hayo maandazi yenye umbo la pembe tatu ama nne lakini niya mviringo na malani zaidi.

Tatizo langu lipo kwenye kiasi gani cha hamira na unawacha kwa muda gani mpaka uumuke.Ukichanganya unga na maziwa au maji uwe mwepesi kiasi gani kwasababu ni unachota na kijiko unatumbukizia kwenye mafuta,tofauti na mengine unasukuma kama chapati halafu ndiyo unakata kwenye umbo unalotaka.

Nikishindwa nitatafuta recipe huko nilikoyala.
 
Back
Top Bottom