Mkuu X-PASTER hakuna mapishi ya kalimati katika ukumbi huo, kama unafahamu jinsi ya kuzikorofisha basi naomba uweke details
Kaimati
Vipimo:
Unga ---------------------2 vikombe vya chai
Hamira ---------------------1 ½ Kijiko cha chai
Samli ---------------------1 Kijiko cha Supu
Maji ---------------------1 ½ kikombe cha chai (kiasi)
Mafuta ya kukaangia --------------------- kiasi
Shira ---------------------1 kikombe
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
1. Changanya unga Hamira, Samli, maji, kisha vuruga kulainisha unga hadi uwe hauna madonge na mwepesi kiasi.
2. Funika unga uumuke. Ukiuumuka (ukifura) choma kaimati katika mafuta ya moto.
3. Ziepue na zichuje mafuta.
4. Weka kaimati katika bakuli au sahani kisha mwagia Shira zikiwa tayari.
Shira:
Sukari --------------------- 2 vikombe
Maji --------------------- 1 kikombe
Zaafarani ---------------------1 kijiko cha chai
Hiliki --------------------- ¼ kijiko cha chai
Arki (rose flavour) --------------------- 3-4 matone