Msaada jinsi ya kuanzisha Consultancy Firm

Baba Ziro

Senior Member
Joined
Apr 15, 2011
Posts
130
Reaction score
30
Habari wana Jamii Forum, naomba msaada wa kuanzisha ofisi Ushauri Elekezi wa mambo ya Kilimo na biashara ya Kilimo kwa ujumla. Ushauri please
 
nadhani unaweza sajili kama kampuni brela. njoo tukutengenezee memorundum and article of
association
 
Kiongozi kusajili Consultancy firm ni kitu cha Dakika 30 tu. Kwanza andaa Jina lako LA biashara. Ingia kwenye website ya Brela na usajili Business name online. Ukishamaliza kusajili jina na likapitishwa basi utalipia kiasi kidogo cha pesa kukamilisha usajili wako. Baada ya hapo utatumiwa Certificate of registration kwenye account yako ya Brela na wewe utakidownload. Hatua inayofuata ni kutafuta office, ukishapata mkataba wa pango nenda TRA ukachukue TIN number, baada ya kupata TIN namba nenda office ya Halmashauri/Jiji kwa Afisa biashara kuomba Leseni, atakupa form Utajaza then ukimaliza Utaenda TRA ambapo watapokea form ya biashara na kupanga kuja kutembelea Ofisi kukukadilia Kodi yako. Basi unaanza kula vichwa.
 
Unamda gani tangu uanze Ku operate hii consultancy firm?
Unataka unataka i operate kitaifa au kimkoa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…