Kiongozi kusajili Consultancy firm ni kitu cha Dakika 30 tu. Kwanza andaa Jina lako LA biashara. Ingia kwenye website ya Brela na usajili Business name online. Ukishamaliza kusajili jina na likapitishwa basi utalipia kiasi kidogo cha pesa kukamilisha usajili wako. Baada ya hapo utatumiwa Certificate of registration kwenye account yako ya Brela na wewe utakidownload. Hatua inayofuata ni kutafuta office, ukishapata mkataba wa pango nenda TRA ukachukue TIN number, baada ya kupata TIN namba nenda office ya Halmashauri/Jiji kwa Afisa biashara kuomba Leseni, atakupa form Utajaza then ukimaliza Utaenda TRA ambapo watapokea form ya biashara na kupanga kuja kutembelea Ofisi kukukadilia Kodi yako. Basi unaanza kula vichwa.