Msaada: Jinsi ya kufika Meatu (Simiyu)

Msaada: Jinsi ya kufika Meatu (Simiyu)

Panda gari hadi singida, utalala singida coz gari za meatu hutozikuta zinaondoka mapema, kesho yake zinaanza safari saa tatu asubuhi, utafika saa 9 au 8 mchana, waweza enda hdi shinyanga mjini utafika usiku sana na utalala pia, hadi kesho yake tena ndo utapata gari za meatu, ila kupita hadi shinyanga kumezunguka sana. Minada mikubwa ni mwanhuzi, bukundi na munhunze iko kishapu .
 
Huwezi fika meatu kwa siku moja lazima ulale tu njiani, singida utafika 11 au 12 jioni na shinyanga utaingia 2 - 4 usiku
 
Ukikutana Na Wenyeji Ukiwaambia Unakwenda Meatu Inakuwa Ngumu Kukuelekeza
Ukisema Njia Ya Kunifikisha Mwanhuzi Unaonyeshwa Haraka

IItilima Maarufu Sana Ingangabilili
Kawaida sana

Ni kama Bukoba vs Kagera,Musoma vs Mara
 
Panda gari hadi singida, utalala singida coz gari za meatu hutozikuta zinaondoka mapema, kesho yake zinaanza safari saa tatu asubuhi, utafika saa 9 au 8 mchana, waweza enda hdi shinyanga mjini utafika usiku sana na utalala pia, hadi kesho yake tena ndo utapata gari za meatu, ila kupita hadi shinyanga kumezunguka sana. Minada mikubwa ni mwanhuzi, bukundi na munhunze iko kishapu .
Huko sahihi
 
Huwezi fika meatu kwa siku moja lazima ulale tu njiani, singida utafika 11 au 12 jioni na shinyanga utaingia 2 - 4 usiku
Siku hizi kina Katarama wanaondoka Dar saa 3 usiku, Shinyanga unaingia mapema asubuhi
 
Panda Allys Bus ya Bariadi au gari zinazoenda Musoma Utashuka Maswa hapo utapata Gari za Meatu

Lakini unaweza kufuata ushauri wa mdau hapo juu, Bariadi kuna mnada mkubwa wa mifugo pia
Tena nitampokea mgen nipo maswa aje na maokoto ya kutosha tukatembee mnadan...kuna bariadi kuna mnadan senani, kuna maswa hapahapa... Kuna mhunze kishapu ...karibu sana mgani
 
Wadau,

Naomba muongozo, nataka kwenda Meatu Dc, mkoa wa Simiyu kuangalia fursa ya mifugo. Mabasi gani nipande kutokea Dar to Meatu na ni masaa mangapi yanachukua? Pia kijiji gani kuna mnada mkubwa wa mifugo?

Asanteni.
Kwa nionanvyo mimi panda bas hadi Dodoma, unaweza ondoka na mabasi ya usiku saa 3 au saa 4,,, saa 12 asbh utakua Dodoma hapo pana basi linaitwa Turu best/Tunda linaenda moja kwa moja mpaka Meatu ,japo sio luxury ila ndio linaloenda huko, alternative unaweza kupanda basi la usiku mpaka Shinyanga ukasubiria hilo bas la Turu au unaweza ukapata mengine huko
 
Wakuu mmempa ushauri mzuri bila kuleta porojo tulizozoea hapa JF kwa niaba yake nawashukuru sana.

Binafsi nimefika huko mwezi uliopita.
 
Akiondoka na basi la usiku anafika singida alfajiri then anaunga na basi la meatu asubuhi hiyohiyo.
 
Kama uko Dar au moro,panda gari hadi Singida mjini.Telemka singida Misuna stendi,panda gari za kwenda Bariadi kupitia meatu Mjini.

Kama uko Arusha au Tanga,panda gari hadi katesh.Pale kuna gari ya moja kwa moja kwenda Meatu kupitia Haydom na Nduguti.
Kama uko nyanda za juu kusini,panda gari hadi shinyanga mjini.Panda gari za kwenda Bariadi ndo urudi Meatu.
Au panda gari hadi Mwandoya,halafu panda gari hadi matu.
Hapo umefika
 
Ahsante sana mkuu kwa kuwa wa msaada!
 
Panda gari hadi singida, utalala singida coz gari za meatu hutozikuta zinaondoka mapema, kesho yake zinaanza safari saa tatu asubuhi, utafika saa 9 au 8 mchana, waweza enda hdi shinyanga mjini utafika usiku sana na utalala pia, hadi kesho yake tena ndo utapata gari za meatu, ila kupita hadi shinyanga kumezunguka sana. Minada mikubwa ni mwanhuzi, bukundi na munhunze iko kishapu .
Mkuu kuna umbali gani kutoka Meatu mpaka Kishapu, kama nia yangu ni minada hii?
 
Ahsante sana Ndugu zangu nimepata mwanga mkubwa. Nachoitaji zaidi ni mifugo, na Je Bariadi na Meatu wapi panafaa zaidi kwa kupata mifugo mingi?
Una million ngapi mkuu ngombe za kisukuma Ni bei pia
 
Back
Top Bottom