usijali mkuu naelewa kama haudeal na hujawahi kukutana na hizi kazi kidogo changamoto ..drill hata ya kukodi tuu kwa fundi ile ndogo , ila kama ni ngumu kuipata Fanya iv ;
-Nunua msumali wa zege wa 4 inchi mmoja tuu , sidhani hata kama unafika 200/= tsh ..
-then kwenye ile level uliyopima unataka iyo TV ikae , chukua ile bracket inayobeba TV Fanya kucholea kwenye ukuta Yale matundu ya screw either kwa pencil au huohuo msumari
-then ondoa bracket , kwenye izo alama chukua nyundo na huo msumali anza kutoboa ayo matundu ..ukimaliza chukua fisha zako then chomeka kwenye izo shimo ulizopata .
-then chukua bracket yako ifunge , cheki kama imekaa poa , bandika TV yako ..hamna cha ajabu boss
Nb: gharama ya misumali na fisha mpaka kazi inaisha sidhan hata kama afu 3 itaisha ..