Msaada: Jinsi ya kulima shamba jipya

Abie

JF-Expert Member
Joined
Jul 15, 2021
Posts
289
Reaction score
535
Wakuu salaam, katika harakati za kutafuta maisha, nimeona niingie shambani.

Swali langu: Inawezekana kwa shamba jipya ukapanda either ufuta au mahindi bila kulima? Yaani ukakata msitu, ukasafisha na kupanda mazao bila kukatua au kuweka matuta? Inawezekana? Na mazao yakakua vizuri tu?

Naombeni muongozo wenu katika hili.
 

Unasafishaje bila ya kuondoa hata kidogo mizizi ya mimea uliyoikuta?

Ni sawa na kutaka kutembea bila ya kunyanyua miguu.
 
Unalima sehemu gani?
Kuna maeneo mengi hasa mkoa wa Pwani maeneo ya kusini kuelekea mikoa yote ya kusini wanakata msitu wanachoma na kupanda ufuta na/au mahindi kama ulivyosema hakuna shida zaidi ya kusumbua mafukutu/machipukizi ya visiki wakati wa palizi.
Watu wanavuna vizuri tu hasa ufuta.

Kwa mahindi ukitaka mavuno mazuri zaidi ng'oa visiki ila uandae pesa nyingi sana kwa kazi hiyo.
 
Asante kwa majibu mazuri. Nalimia Namtumbo,Ruvuma mkuu
 
Mie mwenyewe nataka nifanye kama wewe mwaka huuu.Nimeshauriwa na wenyeji kuchoma na kokomolea mahindi bila kulima, ila mwaka wa pili kulima lazima na mbolea kidogo.

Kuna kipeperushi cha upandaji wa mahindi na maharage bila kulima ninacho ntakutumia upate uzoefu. Wanaita kilimo cha matandazo, kimeandaliwa na taasisi ya utafiti ya uyole.Ngoje nifukunyue makabeasha.
 
Dah! Ntakushukuru sana kiongozi. Unalimia wapi?
 
Aina hii ya kulima bila kukatua nimeiona nilivyokuwa Lindi, kilimo hiko kinategemea unalima mazao gan, ufuta, mbaazi, kunde ndio yanafaa zaid
 
Aina hii ya kulima bila kukatua nimeiona nilivyokuwa Lindi, kilimo hiko kinategemea unalima mazao gan, ufuta, mbaazi, kunde ndio yanafaa zaid
Ahaa sawa , vipi mahindi hayakubali kwa kilimo hiki?
 
Ahaa sawa , vipi mahindi hayakubali kwa kilimo hiki?
Mahindi yanakubali vizuri sana. mchawi mvua tu. Ardhi ikianza kuchoka baada ya misimu mitatu au palizi zikisumbua unahitaji matuta au trekta hapo lazima uondoe visiki n.k.
 
πŸ€“πŸ€“πŸ€“πŸ€“πŸ€“ ""bongo ndo walivo, makamasi tu,""
 
Unalimia mahindi?
Jipya. Ntalima mahindi. Ardhi ni virgini land imejaa matamahuluku, yani hata mtoto anailima.
Nitachoma na kupanda.Ni ardhi nzuri sana. Nchi hii ina ardhi nyie!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…