Mhafidhina07
JF-Expert Member
- Aug 1, 2014
- 3,340
- 4,659
Habari zenu wanajamvi leo ningependa kufundishwa njia zitakazo niwezesha kuwa mtu wa kujiamini niwapo mbele ya watu.
Nasikitika sana juu ya tatizo hili ambalo toka utotoni mwangu hii nimegundua jinsi malezi yangu yalikuwa ndiyo chanzo cha kupungua kujiamini kwani nilikuwa napigwa sana hivo kuuliza kitu ama kuongea ilikuwa ngumu kwangu hivo mpaka sasa nimekuwa muhanga mkubwa.
Naomba kujuzwa mbinu zitakazonifanya niwe bora zaidi katika kujiamini,
Kwani now najiandaa kwenda chuo nikiwa na tatizo hili ndani ya kichwa changu.
ahsante kwa maoni yajiusiwe unaangalia watu usoni pindi unapoongea hii nayo itakusaidia kidogo
zingine ngoja waje masaikolojisti
Hivi vitabu huwa vinapatikana wapi?Ni confidence, siyo ulivyoandika wewe.
Soma kitabu cha Dale Carnegie "How to win friends and influential people" kitakusaidia sana kupita maelezo. Kitabu hicho ni my all time favorite kati ya vitabu vya "how to...".
tayar shida ila huwa natetemeka sana.Umeshawahi kutongoza/zwa tuanzie hapo kwanza.
gud mkuuPole sana mkuu.
Mpaka hapo natumai tayari umeshaanza kufanikiwa katika safari yako ya kutatua tatizo lako kwasababu tayari umeshajua ni kipi kiini cha tatizo.
Mimi ninacho kushauri aanza kujiamini kuazia sasa,na pia jiupushe sana na kujilinganisha na watu wengine kwasababu moja ya sababu ambazo zinasababisha watu wapoteze confidence ni kujilinganisha na watu wengine.
Kitu kingine amini kwamba uwezo wako katika kujua vitu flani unaweza kuwa mkubwa kuliko vile wewe mwenyewe unahisi,kwa mfano unaweza kuwa unajua kitu darasani lakini kwakuwa unadhani kuna watu wanaweza wakawa wanajua zaidi yako ukakaa kimya kumbe katika uhalisia wewe ndiyo unajua zaidi ya wengine........
( Unaweza ku Google kitu kinaitwa imposter's syndrome utanielewa ninacho maanisha)
mh mm ni muislam haturuhusiw wala sitak kujaribHilo ni tatizo kubwa kwa wa tz. Ndio maana watu Wengi wanakuwa walevi vyuoni. Kama ukshindwa kabisaaaa jaribu viroba kila unapopata kusimama mbele ya watu. Rejea, kitwanga.