Wadau wameongea mengi mazuri. Binafsi, hilo tatizo nilikuwa nalo, lakini sasa limepungua kwa 95%. Nilipewa tips zote, hazikunisaidia. Nilichoamua ni kujitatmini mwenyewe. Mara ya kwanza, niliamua kutumia hasira. Yani, nikishakuwa nimezungukwa na watu wanaonitazama, lazima nijikumbushe makusudi kitu kinachoniudhi, maana fact ni kuwa aibu mara nyingi, kama si zote, itakupelekea ucheke au utabasamu, na ukicheka au kutabasamu, utaonekana tu kuwa una aibu. Sasa, hapo nikishakuwa na hasira, nakuwa serious, ila naepuka kuonesha uso wa hasira bhasi siwezi kucheka bila sababu. Hapo naweza kupresent part yangu na nikakaa mbele ya darasa hata lisaa zima bila kuonesha aibu. Baadaye, aibu ikapungua kwa kiasi kikubwa kwa njia hiyo, nikajikuta nazoea mikusanyiko.
Baadaye, nikaamua kuachana na hiyo, nikaanza kukaza macho kwa yeyote atayeniangalia hadi aone aibu yeye. Nikigundua unanitolea macho, mimi nakuangalia mwanzo mwisho, hata kama ni dakika 2, lazima utakwepesha mwenyewe, either kwa kuangalia chini au pembeni. Hapo nishakuwa na confidence, huwezi rudia tena. Nikiona mbishi kuona aibu, naweza hata nikaonesha ishara (facial expression) fulani, kama kunyanyua nyusi. Ukicheka, nimemaliza.
Kwenye presentation, huwa nafanya uhakika kazi nimeielewa vizuri. Assignment nilikuwa napenda kuandaa mimi (kugooglekutype nk), ili siku ya kuwasilisha niwe comfortable, nipate marks nzuri binafsi. Swali lolote litakaloulizwa na audience, nilijibu accordingly. Sometimes nilikuwa najiandaa kwa kusoma grammar kidogo nipunguze broken. Nilikuwa navaa vizuri hadi niamini nimependeza siku ya presentation. Hakikisha upo smart kila idara.
Kwenye group discussion nipo kuna changamoto. Hapo mpo jinsia tofauti, na kama ni mwaka wa kwanza hamjui wenzako. Kuna wajuaji, washushuaji, attackers, wapenda sifa, nk. Sasa hapo lazima uwe vizuri psychologically, kuwa normal, usiact toa point zako au hoja yako na itetee. Hapo aibu unaweza kuiondoa kwa kuzuga na simu tu, kujifanya unagoogle, unachat, au unasoma text, nk. (Sasa simu inasaidia). Ukiona mtu anakukodolea macho, hasa wa jinsia jirani, na wewe mwangalie mwanzo mwisho, akizid mkonyeze. Nilijikuta nakuwa confident hata kwenye course tunazoshea, kama development studies tupo kwenye hall kubwa takribani watu 200, naweza nyanyua mkono ili niulize au kujibu swali nikiwa back bencher. Marafiki zangu wakawa wananikataza eti "nawashazisha," wakawa wanaona aibu wao tena.