wadau wameongea mengi mazuri,binafsi hlo tatzo nilikuwa nalo lakini saiv limepungua kwa 95%,mimi nilipewa tips zote hazikunisaidia,nilichoamua ni kujitatmini mwenyewe.mimi mara ya kwanza niliamua kutumia hasira yani nikishakuwa nimezungukwa na watu wanaonitazama bhasi lazima nijikumbushe makusudi kitu kinachoniudhi maana fact ni kuwa aibu mara nyingi kama si zote itakupelekea ucheke au utabasamu na ukicheka au kutabasamu utaonekana tuu kuwa una aibu.sasa hapo nikishakuwa na hasira kias nakuwa serious ila naavoid kuonesha usoni hasira bhasi siwezi kucheka bila sbabu,hapo naweza kupresent part yangu na nikakaa mbele ya darasa hata lisaa zima bila kuonesha aibu.badae aibu ikapungua kwa kias kikubwa kwa mbinu hyo nikajikuta nazoea mikusanyiko.
badae nikaamua kuachana na hiyo,nikaanza kukaza macho kwa yeyote atayeniangalia hadi aone aibu yeye.nikigundua unanitolea mimacho na mimi nakuangalia mwanzo mwisho hata kama ni dkk 2,lazima utakwepesha mwenyewe either kwa kuangalia chini au pembeni,hapo nishakuwin confidence huwez rudia tena.nikiona mbishi kuona aibu naweza hata nikaonesha ishara(facial expression)fulani kama kunyanyua nyusi,ukicheka nimemaliza.
kwenye presentation huwa namake sure kazi nimeielewa vizur assignment,nilikuwa napenda kuandaa assignment mimi(kugoogle😀😀kutype nk) ili siku ya kuwasilisha niwe confortble,nipate maks nzuri individually,swali lolote litakaloulizwa toka kwa audiance nilijibu accordingly,sometimes nilikuwa najiandaa kwa kusoma grammar kidogo nipunguze broken,nilikuwa navaa vizuri hadi niamini nimependeza siku ya presentation,make sure upo smart kila idara.
kwenye group discussion napo kuna challenge,hapo mpo jinsia tofauti halafu kama ndo first year hamjuani,kuna wajuaji,washushuaji,attacker,wapenda sifa nk.sasa hapo lazima uwe vzuri psychologically,kuwa normal usiact toa point zako au hoja yako na itetee,hapo aibu unaweza kuitoa kwa kuzuga na simu tuu,unajifanya unagoogle,unachati,au unasoma text nk(saiv simu inasaidia) ukiona mtu anakukodolea macho hasa wa jinsia jirani;na wewe mwangalie mwanzo mwisho,akizid mkonyeze😀😀.nilijikuta nakuwa confident hata kwenye course tunazoshea kama development studies tupo kwenye hall kubwa takribani watu 200 naweza nyanyua mkono ili niulize au kujibu swali nikiwa back bencher,marafiki zangu wakawa wananikataza eti "nawashazisha" wakawa wanaona aibu wao tena.