Msaada Jinsi ya kupata gharama za gari iliyoingia toka nje kabla ya kufika TRA

Msaada Jinsi ya kupata gharama za gari iliyoingia toka nje kabla ya kufika TRA

Myelife

Senior Member
Joined
Dec 31, 2011
Posts
164
Reaction score
107
Ndugu wana jamvi, naomba mwenye mawazo ya kunisaidia anisaidie tafadhali, hivi karibuni nimeanza kazi ya u agent wa magari yaliyotumika toka Nje hasa Japan, lakini wateja wengi wanauliza je ni gharama kiasi gani naweza kulipa kama ushuru wa forodha baada ya kulipa shipping (CIF)?
nimetembelea mtandao wa TRA nimepata file fulani la kuweza kumsaidia mteja kukokotoa mahesabu ya gari bila kufika ofisini kwao, nimejaribu kuwaona maswahiba zangu kunisaidia kuchanganua lakini nao wanasema hawako fiti katika suala hili, sasa kwa kuwa JF ni zaidi ya kamusi nimeona niilete kwenu wanajamvi ili nipate uelewa wa jambo hili nami nitakuwa nimerahisisha biashara yangu japo kuna vikwazo vingine lakini mwanzo najua huwa hakuna jambo rahisi.

kwa taarifa zaidi mfano gari Suzuki Carry, FOB dola 700, CIF dola 1800, ya mwaka 1996, cc 660, Milleage 83,000, tutumie mfano huu kwa kupata ukokotozi mzuri,

nimeambatanisha file kotoka katika TRA katika post yangu pia angalizo msisahau kunipa uhusiano uliopo kati ya excell sheet no 1 na excsell sheet no 2

na kwa wanaotumia simu summary ya hizi faili ni kama ifuatavyo

sheet no 1.jpg

sheet no 2.jpg

------------Mwisho----------
 

Attachments

Mdau ni PM niwe na kukokotolea kupitia system ya ASCYUDA ya TRA ipo very accurate ukiachilia na hiyo excel sheet yao.
 
Back
Top Bottom