Msaada: Jinsi ya kupata mkopo kwa dhamana ya nyumba

Msaada: Jinsi ya kupata mkopo kwa dhamana ya nyumba

nimejiajiri mwenyewe mkuu

Mikopo ya benk siku hizi ni majanga inabidi upate elimu kwanza. Na ujiridhishe kabla ya kufikia uamuzi wa kuweka bondi nyumba yako nimeona watu wamekimbia maduka yao wengine nyumba zao kupigwa mnada kwa kushindwa kurejesha mikopo labda kiasi utakachokopa kisiwe kikubwa .
 
jamani ndugu zangu naomba msaada namna ya kupata mkopo kwa dhamana ya nyumba ambayo haina hati yaani skwata
Kaka nenda ofisi ya serikali za mitaa waulize kama eneo unaloishi liko kwenye mradi wa leseni za makazi kama ndio wambie wakupe fomu ya maombi pia watakuelekeza na taratibu zingine. Ukishapata leseni ya makazi nenda azania bank watakupa mkopo, la kama eneo unaloishi halimo kwenye mradi wa leseni za makazi basi hapo itabidi upime na upate hati nenda halmashauri ya manispaa husika idara ya mipango miji kwa msaada...ukifanikiwa kukopa hela
Njoo tukeshe bar...kilala kheri.
 
Kopa kwasababu maalum

Chk

BOYCOT MKUU
 
Zuzu Kachukua Mkopo Benk Kaenda Kaumwaga Mezani Wote Huku Kalewa Kajisahau Mlango Kacha Wazi Waizi Wakapitanao Wote
Katoka Aaha Hawa Wazi Wemechukua Hela Zote Aah Sina Shida Hela Yenyew Nimechukua Mkopo Benk Hahahaha
Jichunge Mzee Bora Ukope Atakama Ni Tasisi Izi Ndogo Ndogo Benk Uki Sua Sua Tu Wata Kukomba Kila Kitu Urudi Kijijini Ukalime ,na Kukata Mkaa.
 
jamani ndugu zangu naomba msaada namna ya kupata mkopo kwa dhamana ya nyumba ambayo haina hati yaani skwata
Kuna aina nyingi za mikopo ungeelezea vitu vifuatavyo ili niweze kukupa njia rahisi ya kuweza kupata
1. Kiasi cha mkopo unaoitaji?
2. Dhumuni la kuchukua huo mkopo?
3. Thamani ya dhamana uliyonayo?
4. Unatumia bank gani?
5. bank statement yako inaonesha turnover ni kiasi gani?
6. Je unafanya biashara au ndio unataka uanze biashara kwa huo mkopo? n.k
 
Mkopo ni majanga


Duuuhh, mbona umetumia lugha kali sana.

Kwa kiasi kikubwa mikopo hasa katika nchi za dunia ya Tatu ina riski kubwa sababu sheria, kanuni na taratibu hazifuatwi barabara. Lakini hiyo si jambo la kutukatisha tamaa.

1. Ni vizuri ukafuata masharti ya mkopo. Mfano usichukue mkopo kwenda kuanzisha biashara.

2.Jambo lolote ili lifanikiwe linanitaka "dhamira"
3.Ni vizuri kuhakikisha una taarifa sahihi juu ya aina ya mkopo unaochukua.
 
Back
Top Bottom