Fuata utaratibu huu;
1. Mchinje.
2. Mtie katika maji ya moto,kwa muda usiopungua dakika kumi.
3. Mtoe na uanze kumnyonyoa,hakikisha unatoa manyoya yote makubwa.(yanayoonekana kiurahisi).
4. Mpake unga na umsugue polepole au mbanike kwenye moto wa mkaa (ili kuondoa mabaki ya vinyoya vidogodogo).
5. Mpasue tumbo mtoe vya ndani kama huwa huli kama unakula vitoe na uvisafishe.
6. Katakata vipande tenga jikoni bila kuongeza maji,mpike hadi akauke kama anataka kuungulia.
7.Badilisha chombo cha kupikia then tia maji endelea kupika kawaida hadi aive kisawasawa.
8. Malizia kwa manjonjo yako tayari kwa kula.