Msaada jinsi ya kupika bata

Mkuu kila mpishi na namna yake, mi sijawahi kutumia hio yako ila ntajaribu. maana nafuga bata home
Kuoka ni sawa.. Kama una oven... Lengo ni lilelile, kwamba nyama ya bata inamaji mengi sana.. Hivyo lazima aokwe au kama unaishi kwa mtogole na hauana oven, basi njia ni hizo nilizozitaja...
 
Wewe mmasai na bata wapi na wapi?
Subiria tukitaka kuchinja ng'ombe ndipo uje kutoa huu uzushi wako!
 
hapo utakaa nje hadi akaukemaana KUNGURU WAKE SI MCHEZO, unaweza kimbizana nao hadi KAWE
Kunguru wanaweza kupeleka mpaka mlandizi.
Isitoshe jamaa anaongea kwa asicho kifahamu.
mimi nafuga bata, nachinja hapo hapo na hapo hapo bata anapikwa vizuri kabisa na analiwa kama kawaida. Sasa yeye hii njia ya kuanza kumshindisha juani bata wa watu kaitoa wapi?
 
Fuata utaratibu huu;
1. Mchinje.
2. Mtie katika maji ya moto,kwa muda usiopungua dakika kumi.
3. Mtoe na uanze kumnyonyoa,hakikisha unatoa manyoya yote makubwa.(yanayoonekana kiurahisi).
4. Mpake unga na umsugue polepole au mbanike kwenye moto wa mkaa (ili kuondoa mabaki ya vinyoya vidogodogo).
5. Mpasue tumbo mtoe vya ndani kama huwa huli kama unakula vitoe na uvisafishe.
6. Katakata vipande tenga jikoni bila kuongeza maji,mpike hadi akauke kama anataka kuungulia.
7.Badilisha chombo cha kupikia then tia maji endelea kupika kawaida hadi aive kisawasawa.
8. Malizia kwa manjonjo yako tayari kwa kula.
 
Hivi ni kweli ukimnyonyoa ukamuacha kidogo,manyoya yanaota mengine? Au uzushi tu
 
Asante mkuu nimekupata
 
Asante sanaa [emoji179]
 
Fata njia zote, lakin ushauri huu wa kumchemsha bila kumkausha achana nao, iyo nyama hautaila. Bata ana shombo flani na kaarufu kabaya sana, kanaishaga mpaka umkaushe kwanza kwa oven au ata mkaa, taratibu moto mdogo at least masaa 3.
 
Aisee nomaa,sasa inabidi umfanyaje ili upate nyama isiyo na vimanyoya [emoji30]

Tafuta kwenye supermarket kitu inaitwa "duck wax". Ndio suluhisho la vinyoya vidogo. Unampaka hiyo wax baada ya kumnyonyoa manyoya makubwa. Unamuweka kwenye freezer, wax ikiganda unaibandua, inatoka na vinyoya vidogo vyote. Wax hiyo ni re-usable.
 
Nyama ya mbele ya bata ni kavu halafu ya nyuma ina mafuta! Upishi wake ni kama kuku tu,ila usimchemshe bila kumkausha kidogo..sio kwamba hatalika la hasha! Ila ile taste itakua tofauti kidogo.. BTW mpe hongera dogo kwa ushindi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…