Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Clips ndo nn baba. G
Crisp au kiswahili cha kwetu kripsi
Makwaru
Ni suala jepesi.
1. Menya viazi/ndizi zako,
2. kata slesi nyembamba. Ni vizuri kutumia kifaa maalumu cha kukatia slesi nyembamba,
3. osha kwa maji safi,
4. weka chumvi kiasi kidogo kisha loweka kwenye maji (yawe usawa na viazi/ndizi zako) kwa muda wa dakika 20,
5. mwaga maji uliyolowekea,
6. weka mafuta kwenye kikaango kisha bandika jikoni, yakipata joto la kutosha weka slesi zako na anza kukaanga ukizigeuza mara kwa mara. Usisahau kunionjesha jaribio lako la kwanza.
Mahitaji
Viazi mbatata kiasi.
Chumvi kiasi.
Mafuta ya kupikia .
Mashine ya kuparuzia karoti (grating machine)
Namna ya kupika
Menya viazi vyako , kisha vioshe vizuri.
Hakikisha hauuachi na majimaji Unahitaji kuwa na kile kimashine kidogo cha kuparuzia nyanya au karoti(grating machine) au kama huna waweza kutumia kisu kukatakata katika maduara membamba
Vianike kidogo viwe vikavu,weka mafuta, wacha yapate moto. Vimimine ndani ya mafuta,uvikaange
Geuzagauza visishikane.
Wacha mpaka viwe rangi ya hudhurungi
ipua nyunyuzia chumvi , wacha vipoe.
Tayari kwa kuliwa