Msaada: Jinsi ya kupika Crips nzuri

Msaada: Jinsi ya kupika Crips nzuri

Baba.G

New Member
Joined
Aug 31, 2015
Posts
1
Reaction score
0
Ni njia zipi zunatumika katika kuaandaa clips nzuri na yenye kuvutia. Isiyoungua. Hasa clips ya viazi.
 
Menya viazi vioshe
Kwangua na kikwangulio (hapa ndio pana changamoto. Baadhi ya vimashine sio vizuri sana hufanya viazi kuwa vinene na crips hazitoki vyema)

Weka mafuta kwenye karai yakipata moto wa kutosha (yasiwe makali sana wala yasiwe makali kidogo)

Weka viazi vyako...geuza geuza visiungue

Ipua kwenye chombo

Tia chimvi au pilipili

Fungasha
 
Ni suala jepesi.
1. Menya viazi/ndizi zako,
2. kata slesi nyembamba. Ni vizuri kutumia kifaa maalumu cha kukatia slesi nyembamba,
3. osha kwa maji safi,
4. weka chumvi kiasi kidogo kisha loweka kwenye maji (yawe usawa na viazi/ndizi zako) kwa muda wa dakika 20,
5. mwaga maji uliyolowekea,
6. weka mafuta kwenye kikaango kisha bandika jikoni, yakipata joto la kutosha weka slesi zako na anza kukaanga ukizigeuza mara kwa mara. Usisahau kunionjesha jaribio lako la kwanza.




Mahitaji
Viazi mbatata kiasi.
Chumvi kiasi.
Mafuta ya kupikia .
Mashine ya kuparuzia karoti (grating machine)

Namna ya kupika

Menya viazi vyako , kisha vioshe vizuri.
Hakikisha hauuachi na majimaji Unahitaji kuwa na kile kimashine kidogo cha kuparuzia nyanya au karoti(grating machine) au kama huna waweza kutumia kisu kukatakata katika maduara membamba
Vianike kidogo viwe vikavu,weka mafuta, wacha yapate moto. Vimimine ndani ya mafuta,uvikaange
Geuzagauza visishikane.
Wacha mpaka viwe rangi ya hudhurungi
ipua nyunyuzia chumvi , wacha vipoe.
Tayari kwa kuliwa


Usisahau kuleta feedback
 
ingekuwa chips ingekuwa ya msaada sana maana wale jamaa wanaokamua transform er wanatutesa.
 
Back
Top Bottom