Msaada!jinsi ya kutoa tatto iliyichorwa na sindano!

cuchi

JF-Expert Member
Joined
Oct 1, 2012
Posts
218
Reaction score
74
Habari wana jamii!

Jaman kwa wale wenye kujua jinsi ya kutoa tatto nahitaj msaada,nina mdogo wangu wa kike 17, leo naamka asubuh naona anatembea kainama hlf kajifunika begani namchukuza kachora tatto began jana anasema hlf mpk inatoa majimaji na imevimba sana!

Naomben msaada wenu nina hasira sana nataman kumpiga ila hyo hali inanitia wasiwasi sana na nin madhara yake! Na pia wazazi wakiona watasema nimeshindwa kumlea mdogo wangu yaan hta kazini sijaenda leo.

Msaada tafadhali.
 
Mkuu pole sana, jaribu kuweka hili bandiko na kule JF DOCTOR waweza pata msaada zaidi.
 
Maoni yangu ni: Kwanza kidonda kitibiwe i.e. aende hospital, halafu baadae inaweza kufutwa kirahisi kabisa kwa kutumia laser.
 
jamani hata mimi nina shida hiyo mkuu ebu tufafanulie kidogo kuhisu hiyo laser, kwani mimi nina tatoo ya miaka mingi.
 
Rahisi sana chukua pasi ya umeme washa subir ipate moto wa kutosha then fanya kama unanyoosha hapo kwenye tatoo, mara moja mara mbili kwisha habari yake.
 
Rahisi sana chukua pasi ya umeme washa subir ipate moto wa kutosha then fanya kama unanyoosha hapo kwenye tatoo, mara moja mara mbili kwisha habari yake.

Hii ndio njia nzuri.
 
huyo atakuwa kapata infection,nina wasiwasi na hivyo vifaa vilivyotumiwa.ni vizuri aende hospitali haraka.
 
Rahisi sana chukua pasi ya umeme washa subir ipate moto wa kutosha then fanya kama unanyoosha hapo kwenye tatoo, mara moja mara mbili kwisha habari yake.

Mmmmmmhhhh nahisi unanitafutia matatizo mengine
 
Laser ndo nin mkuu mi hata nieleweshe

Laser ni chombo... labda niseme kama kalamu kubwa ambayo inatoa ''miali'' (high intensity light beam) inayopenya ngozi na kufuta alama za tattoo kwenye ngozi. Huduma hii hupatikana hospital na hasa kwa ma-dermatologists (specialists wa ngozi) na cosmetic surgery clinics. Nadhani hata Tanzania hii huduma ipo na cost yake sio kubwa sana!
 
Asante mkuu ila ni hospital gan unayofahamu ina huduma hii?pia kuna mtu kanaimbia wine or galric inasaidia
 
Asante mkuu ila ni hospital gan unayofahamu ina huduma hii?pia kuna mtu kanaimbia wine or galric inasaidia

Mkuu, sijui hospital inayotoa hiyo huduma kwa Tanzania, jaribu kufanya uchunguzi na mimi pia nitajaribu kuulizia. Kuhusu kujaribu kufuta kienyeji, kuwa mwangalifu. Unaweza ukasababisha kovu na mambo yakawa mabaya zaidi.
 
aisee pole sana, vijana kwa kuiga wasiyoyajua! mpeleke hospitali ndio suluhisho coz kuna issue ya tetenas hapo
 
aisee pole sana, vijana kwa kuiga wasiyoyajua! mpeleke hospitali ndio suluhisho coz kuna issue ya tetenas hapo

Mmmmmmhhh hilo nalo neno!asante
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…