Msaada jinsi ya kuuliza maswali Mahakamani

Msaada jinsi ya kuuliza maswali Mahakamani

Kuna mwanamke nimeishi nae kwa muda wa miezi 6, mambo yakaharibika baada ya kumkuta na mwanaume chumbani kwake, kukatokea ugomvi wa hapa na pale.

Sasa huyu mwanamke ananishitaki mahakamani kwa kosa la shambulio la kudhuru mwili. Ametakiwa kupeleka mashahidi na ameandaa mashahidi wa kununua ili kunikomoa. Mmoja wa mashahidi ni kuwadi aliyemtafutia bwana.

Naomba wataalamu wa kesi mnipe nondo za maana za kuwauliza hao mashahidi.

Karibuni..
Mashahidi kawatolea wapi? Walikuwepo au ni majirani! Kama ni majirani waulize walisikia shambulio wakiwa nje au ndani.
 
Nakuona mwanasheria Kanjanja unazidi kulaghai majuha wa mitandaoni.

Cross examining is a skill, sio ujinga huu umeandika hapa!

This is not a cross, it is rubbish!

Wakili yoyote hawezi kuuliza huu ujinga atajiharibia kesi yake.
Bora yeye na ukanjanja wake Kuliko wewe na usomi wako,

Sasa umeandika Nini hapa??

Kwamaneno Yako na muuliza swali yanaendana? Kama ungelikuwa unajua si ungetoa Nondo zako tuzione?
 
Nakuona mwanasheria Kanjanja unazidi kulaghai majuha wa mitandaoni.

Cross examining is a skill, sio ujinga huu umeandika hapa!

This is not a cross, it is rubbish!

Wakili yoyote hawezi kuuliza huu ujinga atajiharibia kesi yake.
Much know !!!! Empty
 
kua tu mkweli, kama hauna shahidi usijaribu kuleta shahidi wa bandia, maana yeye ndio anaweza akakuaribia kesi hasa kwa upande wako, ulikua peke ako ivyo simama peke ako, hio pf3 isikuogopeshe mkuu, siku zote mahakamani ukweli unaonekanaga tu.


Toa ushaidi wako, huku ukianza kwanza kuelezea juu ya mahusiano yenu na muda mliokaa pamoja ili ionekane mlikua na mahusiano makubwa sana.
elezea tukio zima lilivyokua, ktk maelezo yako onesha kabisa hukumshambulia mtu kwa kutumia mwili wako au silaha zozote(na hasa ukizingatia wao walisharikologa kwenye ushahidi wao)
elezea tu kulitokea ubishani wa maneno tu hivyo ukaamua uondoke zako, ni kama ungetokea ugomvi wa aina yoyote mkubwa basi wewe ndio ungekua wa kwanza kuzulika kwakua wao walikua wawili yeye na bwana ake(if nilikunote vibaya, ulisema" baada ya
kumkuta na mwanaume chumbani kwake,
kukatokea ugomvi wa hapa na pale.")
au kama alikuepo peke ake sikuio ya ugomvi, basi kana kabisa kumpiga uyo mwanamke hasa ukizingatia alitoa ushahidi dhaifu sana.
Sijiombei kupanda kuzimbani kwa namna yoyote ile iwe kushitaki au kushitakiwa (Mungu aniepushe).
Ila siku ikitokea kwa kudra za Mungu mkuu 666 chata lazima nikutafute unipe mwongozo.
Mungu akubariki sana aisee nimesoma comments zako upo vizuri sana.
 
Sijiombei kupanda kuzimbani kwa namna yoyote ile iwe kushitaki au kushitakiwa (Mungu aniepushe).
Ila siku ikitokea kwa kudra za Mungu mkuu 666 chata lazima nikutafute unipe mwongozo.
Mungu akubariki sana aisee nimesoma comments zako upo vizuri sana.
Jamaa anajua sana sheria aisee
 
Uuulize je wewe ulikua ni nani yake? Ulivyoingia humo chumbani kwake uliwakuta wanafanyaje? (Ukumbuke kisheria uko mahala pazuri kwa kujitetea coz huyo ni mpenzi wako na vile ulivyowakuta ilikua sawa kabisa we kufanya uliyofanya lakin ktk muda huo huo, hii tunaita 'kupandwa na jazba au hasira za ghafla tokana na tukio hasi dhidi yako'.

Maswali hayo mawili kwa huyo mwanamke wako yatakuweka mahala pazuri sana, japo ndani ya maswali haya unaweza pata vingine vya kujiuliza humo humo akiwa anakujibu.

Waulize hao mashaidi, "Je siku ya tukio walikuwepo eneo la tukio? Je, wanaweza isaidia mahakama namna ulivyokua unaonekana kimavazi, n.k.?
Waulize je huo ushaidi wao waliuona au waliskia?.

Endapo ikitokea mmoja wapo akasema aliona, muulize, je anaweza elezea tukio kwa kifupi? Aliwezaje kukuona wewe wakati mlikua ndani? Kama ulimdhuru huyo mwanamke wako ulimdhuru na kitu gani? Wapi? Kama walikuepo eneo la tukio na waliona je walifanya juhudi gan kuzuia shambulizi? Wana uhusiano gani na huyo mfungua kesi?

Waambie kuwa nyie mmeupika huo ushahidi wenu kwa kuwa mnafahamiana na huyo bwana wa mfungua kesi.

Kumbuka usiwe muoga, jiamini, hauwezi kufungwa, na ukiweza unawezaandika haya na yakakuongoza mahakamani vizuri tu kwani inaruhusiwa kuingia na vikaratasi mahakamani vyenye maswali ambayo wewe mwenyewe uliyaandika....

Usiogope.
Mkuu mimi kuna mtu aliniibia simu yangu usiku wa saa tisa nilimuona dirishani( kuna taa imefifia mwanga lakini unaweza kumuona mtu na mlangoni(pale mlangoni kuna ka duara hivi kwahiyo kabla ya kufungua mlango nilimuona na penyewe kuna taa ambayo inamulika vizuri) sasa zikapita siku nikawa namuona sehemu. Ikabidi niende kumshtaki. Wakauliza anapokaa anasema mtaa ule ule ninaokaa mimi, ila kijana akakataa kata kata kwamba siyo yeye, akati yeye ndiye niliyemuona ila anabisha . Basi wakasema kesi ipelekwe mahakama. Ndiyo tunasubiria week ijayo. Vipi ni maswali gani ya kumuuliza mtuhumiwa?
 
Back
Top Bottom