Msaada juu ya biashara visiwa vya ungujah

Jurrasic

Member
Joined
Oct 19, 2018
Posts
67
Reaction score
67
Habarini wanajamvi
Mimi Niko morogoro ilah nilifika tanga mjini soko la mgandini nikakuta magari mengi malori ya Azam yamebeba vitunguu ,makabichi,nyanya na vitu vingine nkaambiwa kwamba vyote vinaenda pemba na Ni mtindo Kila j3 hivyo haraka haraka biashara inaonekana kuwa vizuri huko pemba
Ilah sikuweza fika pemba kujua soko la hizo bidhaa likoje sabab hela nayo Ni tatizo

Ilah sijajua pia ungujah vitu vyao km mboga mboga ,nafaka na viungo vinatokea wapii na soko lake kwa bidhaa za vyakula likoje

Kwa walio wahi fanya biashara ya nafaka,mazao na mboga mboga kwa visiwa vya pemba na ungujah naomba tushare ujuzi

Upande wangu nataka nifanye biashara ila tatizo sifahamu Hali ikoje pia hela ynyw Ni ndogo kiasi kwamba kufanya utafiti mwnyw mtaji unakatika

Wandugu msaada wa taarifa juu ya mwendendo wa biashara na masoko
Natanguliza shukrani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…